Waziri Mkuu, unda tume kuchunguza NBAA!

Joined
Aug 10, 2011
Posts
35
Reaction score
13
Ni hivi majuzi tu Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda aliunda tume kuchunguza sababu za kufeli kwa wanafunzi wa Form Four iliyopelekea kuwa na matokeo mabaya nchi nzima.

Tunakuomba Mheshimiwa Waziri Mkuu kuunda tume nyingine ili kuchunguza kuwepo kwa matokeo mabovu kila mwaka kwa miaka nenda rudi kwa watahiniwa wa mitihani ya CPA (Certified Public Accountant) inayotolewa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa mahesabu (NBAA).

Tunasema kuna umuhimu wa kuunda tume kuchunguza bodi hii kutokana na ukweli kwamba mitihani inayotolewa na bodi hii ni ya kukomoana sana.Lengo lao ni kuhakikisha kwamba wanaopata hiyo CPA wawe wachache mno. Kwa mfano wanaweza wakafanya mitihani hiyo watahiniwa zaidi ya elfu tatu (3,000) lakini watakaopata hiyo CPA ni chini ya watahiniwa mia tatu tu (300).

Sisi wahasibu tunaona bodi hii haikuundwa kuendeleza taaluma hii ya uhasibu bali ni kuididimiza taaluma hii ili kuwe na wahasibu wachache mno wenye sifa za kuitwa wahasibu. Kwa sababu kwa mujibu wa Ndugu Ludovick Utouh ambae ni mkaguzi mkuu wa serikali (CAG) anamtambua mhasibu ni yule mwenye CPA tu. Hawa wengine wanaofanya kazi za uhasibu lakini hawana CPA wanajipendekeza tu na ndio wanaoharibu kazi na sifa za taaluma ya uhasibu.

Bodi hii ya NBAA imejihakikishia maisha ya kifahari kwa kila mtumishi wake kutokana na kukusanya mabilioni ya pesa ya bure kutoka kwa watahiniwa wa mitihani yake.

Kwa mfano hii sheria waliyoiweka ya kwamba Mtahiniwa akifanya mitihani na kufaulu somo moja basi wanalifuta, ni sheria kandamizi yenye lengo la kuwarudisha nyuma watu wanaopenda kujiendeleza katika fani hii na vile vile kuleta aina mpya ya UTUMWA kupitia sekta ya elimu. Yaani mtu atumie robo tatu ya umri wake wa kufanya kazi akiwa anasoma.

Sisi binafsi(Wahasibu) hatuelewi kama mtu somo amefaulu eti kwa kuwa ni moja linafutwa kwa nini ? Wakati mpaka huyo mtu amelifaulu hilo somo ametumia rasirimali chungu nzima ikiwemo Muda,Fedha na Jitihada kubwa mpaka kufaulu somo hilo.

Imefikia mahala waajiri wengi hawataki kuwalipia wala kuwaruhusu wafanyakazi wao kufanya mitihani hii kwa kuwa wameona ni kupoteza muda na rasilimali tu. Mtu badala ya kutumia muda wake mwingi katika kufanya kazi ili kuinua uchumi wa taifa, badala yake anatumia muda mwingi kusomea CPA ambayo kuipata kwake ni mpaka Mabwana wakubwa wa NBAA watakapokuwa tayari kukupa. Tunasikitika sana kuona nchi kama ya Uingereza ambayo imetuacha mbali mno kiuchumi na kimaendeleo kwa ujumla, ukifanya mitihani yao ya ACCA hata kama ni somo moja moja na ukafulu wanali-record na unamalizia mengine yaliyobaki. Lakini kwa NBAA ukifaulu somo moja wanalifuta.

Kwa kumalizia tunakuomba Mheshimiwa Waziri mkuu, usisubiri mpaka kutokee maandamano unda tume kuchunguza utendaji kazi wa Bodi ya NBAA kwani imekithiri kwa kufelisha watahiniwa wake kwa makusudi.
 

Attachments

  • nbaa.jpg
    8.7 KB · Views: 205
MHASIBU HALISI wewe ni muhanga wa shule ya uhasibu na ukaguzi.wengine tulikwisha maliza tunakula good time mitaani.wewe endelea kulia tu na machozi yako yanaenda na MAJI.SUBIRI SYLABUS MPYA ya kurekodi somo moja unaweza kubahatisha nawe ukapat GA.
 
Last edited by a moderator:
Naomba kukuliza MHASIBU HALISI ..........sylabus mpya inaanza kutumika tena lini, nasikia every time the sylabus changes
 
Last edited by a moderator:
MHASIBU HALISI wewe ni muhanga wa shule ya uhasibu na ukaguzi.wengine tulikwisha maliza tunakula good time mitaani.wewe endelea kulia tu na machozi yako yanaenda na MAJI.SUBIRI SYLABUS MPYA ya kurekodi somo moja unaweza kubahatisha nawe ukapat GA.

Nimeipenda hii,.........shkamooooooo!!!!!!!!
 
Kwa upande wangu naiunga mkono NBAA kwa kuhakikisha inatoa watu ambao ni professional,mimi namalizia somo moja la Module F kwa sasa hivi.Kwa kweli mitahani yake inahitaji

maandalizi ya kutosha na uhakika.Aliyetoa mada hii inaonekana ni mtu aliyejaribu kuifanya hii mitihani akashindwa, na naona alidhani ni mteremko,hivi ndo tunataka bodi iwe.Kama umeshindwa nenda masters au kwenye bodi nyingine, hatutaki vihiyo.
 
Ujiitaye Mhasibu Halisi,

Inasikitisha kujiita mhasibu halisi na kutumia nembo ya Bodi ya Uhasibu wakati wewe sio mhasibu kabisa!! Kama unajaribu mitihani na kukushinda, wewe ni karani tu.

Nasema inasikitisha kwa sababu hujui hata majukumu ya Bodi hii NBAA na naamini hujui hata majukumu yako wewe kama mhasibu matarajiwa. Hutaki kusoma kwa bidii, unataka NBAA wakuogope wakupasishe uje kutia aibu taaluma ya wahasibu.

Unataka CPA(T) ya kudunduliza kama vijisenti kwenye KIBOBO!! Hii ni aibu kubwa. Eti ukifaulu somo moja, NBAA wakuwekee kwenye kibobo na ulivyo kilaza hicho kibobo kitajaa lini? Pindi kitakapo jaa utakuwa Mhasibu kweli wewe?

Acha taratibu za BODI zihashimiwe, na wewe soma kwa bidii, soma kwa furaha bila uoga utafaulu tu.

Mh Waziri Mkuu, endelea na majukumu muhimu ya kitaifa, sio kuhangaika na wavivu wa kufikiri, wanaotaka kila kitu walishwe kama makinda ya ndege.

KEEP UP NBAA!!!, Chuja na ulete wahasibu bora sio bora wahasibu
 



Kwa upande wangu sioni tatizo lolote kuhusu NBAA kwani kuna watu ambao wako makini na kile wanacho kifanya na wamefaulu vizuri tu bila matatizo.Tatizo kubwa watanzania ni wavivu na tunapenda sana kulalamika badala ya kufanya kazi.Nina imani watukama hawa hata wakienda Masters au Bodi zingine sidhani kama watafaulu.Tuache kulala mika tufanye kazi.
 
.. mie nabana "------" nimalizie kasomo kamoja kamebaki , ila balaa... Sasa wanareveiw silabasi nisipo chomoa, wananiongezea mengine nindelee kuwachangia !

Balaa kabisa
 
Kama CPA imemshinda, kwa ACCA hata asijaribu kukanyaga maana siku hizi NBAA wenyewe wameishiwa maswali ya kutahini watu wamebakia kucopy na kupest maswali na majibu ya ACCA!!!!
 
Nadhani mpaka utoe rushwa ndio unapewa cpa. Ukisoma MBA na wenye cpa utashangaa wengi wako kaputi na hawamalizi. Sawa kabisa mkuu, iundwe tume huko kuna urasimu wa ovyo kabisa.
 

Mudokanyi wewe ni great thinker!!! Ila nakushangaa kwa kutoa majibu ya kijinga kiasi hicho. Mtoa mada amejitahidi kuelezea vizuri tu kuhusu watu kufeli kwa kiwango cha kutisha lakini wewe eti unasema "hivi ndo tunataka bodi iwe".... ukimaanisha kwamba ili bodi iheshimike ni lazima iwe natoa mitihani migumu na watu wasifaulu kwa kiwango kikubwa. Na eti unasema mtu anayefeli mitihani NBAA ni vema asome Masters ama afanye mitihani ya bodi zingine..... Huu ni udhaifu mkubwa kabisa na ni upungufu wa elimu kichwani. Kama nchi hii inawasomi wanaokurupuka kutoa majibu kama yako basi kumbe ndo maana nchi hii haina maendeleo kabisa. Chukulia wewe ndo ni final wa kutoa suluhisho la tatizo na kumbe ukatoa majibu kama hayo..... unategemea utakuwa umeumiza watu wangapi?
Sasa hebu sikiliza wasomi wenzio walivyotoa maoni yao kuhusu NBAA na mitihani wanayotoa. Tena ni wasomi waliopewa kazi ya kutoa maoni na kubadilisha mfumo na mitaala ya NBAA.....Si wengine bali ni The Institute of Chartered Accountants in England and Wales:

ICAEW has carried out a fullcurriculum-based review of the NBAA professional qualification. The review hascovered a full review of the current professional syllabus, examinationprocesses and procedures, pathways to entry, teaching and learning andpractical work experience requirements. The current syllabus of the CPAqualification was introduced to the classroom in early 2008 and the examinationsunder the new structure started in May 2008.Professional bodies must championthe quality and credibility of their professional qualification. In general theNBAA professional qualification is well regarded. It is however timely for areview against international comparators and benchmarks in a range of areas,including the syllabus and exemption policy, the quality of teaching andlearning and the practical work experience requirements.The NBAA has not been universallythe ‘qualification of choice' for students in Tanzania, due to some loss ofmarket share to international comparators. Our review has therefore alsoincluded the need for brand and marketing on the new NBAA professionalqualificationThis report highlights the keyfindings of our review, including the following selected findingsHeadline observations and findings
Syllabus and assessments
1. The current syllabus lacks an articulated visionof an NBAA professional accountant.
2. Many of the current students find the currentsyllabus and assessments challenging.
3. The current syllabus is a statement of contentrather than required competences.
4. The syllabus lacks progression and is heavy withpapers relative to international comparators.
5. Thecurrent assessments lack the use of business scenarios to measure knowledge andskills.
6. Some core examination topics are not examinedwith sufficient regularity.
7. There is concern that exam questions fall shortsometimes in reflecting syllabus weightings.

Examinationprocedures and rules
8. Modules and papers are taken in sequence and allpapers in a module must be sat.
9. The rules requirestudents to pass two exams before they can keep one.
10. Examination and assessment process
11. The current process is robust and clear.
12. The practice of assembling exams from a bank ofquestions rather than from a single examiner creates inconsistencies.
13. Pathways to entry (credits for prior learning)
14. The process for accrediting institutions forexamination exemptions is light in touch.
15. This creates too big a gap at times andcontributes to low pass rates in examinations.
Teaching and learningprovision
1. The teaching and learning process for studentsis variable in quality.
2. The NBAA recognises the need for improvedteaching and learning provision.
3. Teachingand learning materials
4. Teaching and learning materials are variable inquality and are not specifically geared to the
NBAA exams
1. The adoption of a new syllabus provides anopportunity to create new teaching and learning materials that are fullyintegrated with it.
2. IFACrequirements for IES 1-5
3. Current work experience meets basic IFACrequirements, but doesn't create close collaboration between the NBAA, mentorsand students in creating workplace learning that supports examination learning.
4. Currentsyllabus does not fully embrace the communication and professional skills requirementsof IFAC.
5. Publicand private sector integration
6. Coverage of public and private sectors insyllabus is an essential requirement in Tanzania.
7. NBAA is currently integrating public and privatesector elements into the qualification programme.
8. The brandand marketing of the NBAA and its professional qualification
9. The NBAA brand could be enhanced to attract thebest and brightest students.
10. The qualification is inadequately marketed.

Isome vizuri hii na kujiridhisha kuwa na hawa nao ni "VIHIYO!!!!!!"
 
Wale jamaa wa NBAA nakumbuka walinikamata mara moja tu kwenye Auditing & Investigation. Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kufanya Supplimentary exam kwenye historia yangu ya shule. Usema kweli ile mitihani yao si ya kujenga taaluma bali ya kukomoana. After all they are just copying from ACCA past papers.

TUMBIRI (PhD In Progress, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd [/SUP]Overall Best Student in Form Six National Exams),
tumbiri@jamiiforums.com


Nakala: MHASIBU HALISI, Kimbunga, etc
 
Last edited by a moderator:
Ukilaza shida kweli.Mwache Pinda aendelee na siasa zake na NBAA iendelee kufanya shughuli za kusimamia profession ya uhasibu.Umeshindwa kupata CPA,tafuta vitu vingine vya kufanya,kazi siyo uhasibu tu ndugu yangu.
 
NBAA ni bodi ya ukweli ya uhasibu Tanzania hiyo sio NECTA bwana hyo ni bodi inayotoa cream tupu kama ww ni kilaza huna lako hapo katafute nazi ukune
 
wajinga ndio wanadhani CPA ndio maisha, wajinga ndio wanaringia CPA huku wakipewa wasolve real accounting problems wanashindwa. nina bcom yangu nzuri ya acc nafikiri nahitaji kuendelea kufanya kazi kwa muda nipate uzoefu huku nikipata mshahra mzuri tu, nikitaka kujiendeleza nitasoma MBA na sio CPA ya kupoteza muda na pesa, ndugu jipange, hujasoma mpaka chuo kikuu uje ulalamikie mabwana wa NBAA. Kuna wahitimu kibao wamepata kazi za uhasibu na wanafanya kazi vizuri bila hata ya hizo CPA, usifanye CPA wa determine future yako.
 
mmmhhhh kweli NBAA wanashika sana wapunguze kubana,pia manual za masomo hamna,7bu zipo nyingine za watu kufail paper.Wangekuwa wanafanya kama acca wanavyofanya ingekuwa poa unapewa na nondo zote za kusomea na kujua pia area of concentaration,cpa zingekuwa za kutosha
 

MOSI. Je unaunga mkono hoja ya huyu kilaza ya Waziri Mkuu kuunda Tume?
PILI. Uhasibu siyo ELIMU bali ni FANI kama zilivyo fani za uhandisi, wakili, daktari n.k. Kufeli mitihani ya NBAA ni kukosa msingi imara wa elimu yetu ya juu maana kwanza NBAA haifundishi bali ina 'test' uelewa wa ulichojifunza kwenye elimu yako ya juu. Ndiyo maana aliyemaliza shahada ya uhasibu au advanced diploma ya uhasibu anasamehewa baadhi ya masomo kwa assumption kuwa hayo aliyosamehewa anayafahamu maana alishajifunza. Ambaye akusoma uhasibu kwenye shahada yake hapati msamaha kwa kuwa wanajua hakusoma hivyo inabidi asome.

Kwani huko vyuoni wote wanafaulu kuhalali? Ndo hao hao wanaingia kufanya mitihani ya CPA. NBAA watu wanakwama kwa sababu HAWAHONGEKI. Mbona mimi nimefanya mitihani bila hata kuhudhuria hizi mnaita review classes. Nimetumia notisi zangu na elimu ya chuo na nikafaulu tena kwa sitting mbili tu. Tuache kuhamisha matatizo wakati sisi wenyewe ndo tuna matatizo
 
NBAA siyo bodi ya kubabaisha.na hata CEO wake bw.Pius Maneno ni mtu makini na mwadilifu sana,namfahamu tangu akiwa shuleni pale Sangu.BRAVO NBAAA.KEEP IT UP!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…