Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amelazwa hospitalini ili kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.
Katika taarifa kutoka kwa ofisi yake siku ya Jumapili, Aprili 5, kiongozi huyo bado anaonyesha dalili za virusi vya corona siku kumi baada ya kuthibitishwa kuwa na virusi hivyo.
Waziri Mkuu wa Uingereza , Boris Johnson alipatwa na virusi hivyo mnamo Machi 26.
Ofisi yake pia ilibainisha kwamba kulazwa kwake hospitalini si jambo la dharura bali ni kutokana na ushauri wa daktari wake kama njia ya tahadhari.
Kulingana na ripoti kutoka kwa vyombo vya habari nchini humo, Johnson, mwenye miaka 55, amewekwa karantini katika makazi yake ya Downing St. tangu kupatikana na COVID-19 mnamo Machi 26.
Boris Jonhson amewekwa karantini katika makazi yake. Picha: UGC.
Johnson kupitia video, mnamo Ijumaa, Aprili 3, alisema yuko buheri wa afya lakini bado alikuwa na joto jingi mwilini.
Waziri huyo alisema kukaa nyumbani kunasaidia katika kuokoa maisha na kumhimiza kila mmoja kuzingatia hayo
Rais wa Marekani Donald Trump pia alimtakia Boris heri njema wakati wa hotuba yake ya Jumapili, Aprili 5, kutoka Jumba la White House.
Viongozi kadhaa katika serikali ya Johnson wamepatikana na virusi hivyo akiwemo Waziri wa Afya Matt Hancock na msaidizi wake Nadine Dorries ambapo wote wamepona.
Kufikia siku ya Jumapili, takriban watu 48,000 wamethibitishwa kuwa na COVID-19 nchini Uingereza huku 4,934 wakipoteza maisha yao.