101 East
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 1,057
- 2,221
Waziri Mkuu wa zamani wa Italy na Tajiri namba mbili nchini humo ndugu Silvio Berlusconi amefariki dunia leo hii 12/06/2023
Berlusconi ambaye alikuwa ni mmiliki wa vyombo vya habari na timu ya AC Milan amefariki akiwa na umri wa miaka 86 kwa Ugonjwa wa Kansa ya Damu.
====
Waziri Mkuu wa zamani wa Italy Silvio Berlusconi amefariki dunia, akiwa na umri wa miaka 86. Tajiri huyo bilionea ambaye alikuwa anamiliki vyombo kadhaa vya habari, amekuwa akitibiwa Ugonjwa wa Saratani ya Damu.
Berlusconi alianza kutengeneza utajiri wake katika sekta ya ujenzi wa majumba kisha akaendelea kuunda mtandao wa vituo vya televisheni, akifanikiwa sana katika biashara hiyo. Wakati fulani, alijulikana kama tajiri mkubwa wa Italy.
Mwanasiasa huyo wa mrengo wa kulia alihudumu kama Waziri Mkuu katika serikali nne kuanzia mwaka wa 1994.
Berlusconi alikabiliwa na kashfa nyingi za kisiasa wakati wa maisha yake. Alijulikana kwa karamu zake mashuhuri za bunga bunga kuhusiana na kufanya ngono na makahaba, lakini kashfa hizo hazikumuzuia kujenga urithi wa kudumu wa kisiasa.