Waziri Mwakyembe awateuwa Wajumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT)

Waziri Mwakyembe awateuwa Wajumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT)

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) kwa mujibu wa Sheria ya Baraza Ia Michezo Ia Taifa (BMT) ya mwaka 1967 pamoja na marekebisho yake ikisomwa na muundo wa shughuli za Baraza(Provisions of the Schedule to the Act), amemteua Bw. Leodger Chilla Tenga kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Ia Taifa.

Dkt. Mwakyembe amewateua pia wajumbe wapya sita(6) wa Baraza hila kama ifuatavyo:

1. Prof.Mkumbwa M. A. Mtambo.
2. Bi. Beatrice Singano.
3. KanaliMstaafu Juma lkangaa.
4. Bw.John Joseph Ndumbaro.
5. Bi. Rehema Sefu Madenge.
6. Bw.Salmin Kaniki.

Aidha,Dkt.Mwakyembe amewateua wajumbe wengine watatu (3) wa Baraza kutokana na nafasi za vyeo vyao ambao ni:

1. Yussuph Singe Mkurungezi wa Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
2. Dkt. Edicome Shirima•Kamishna wa Elimu,Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na
Mafunzo ya Ufundi.
3. Mohammed Kiganja, Katibu Mkuu wa Baraza Ia Michezo Ia Taifa ambaye atakuwa ni Katibu wa Baraza.

Uteuziwa wajumbe wote umeanza rasmi tarehe 08 Februari, 2018 na watalitumikia
Baraza kwa kipindi cha miaka mitatu (3).

Vilevile Dkt. Mwakyembe kwa mujibu wa sheria amemteua Bw. Timothy Mganga kuwa
Mkuu wa Chua cha Maendeleo ya Michezo Malya kwa kpi indicha miaka mitano (5).

lmetolewa na Lorietha Laurence
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari UtamaduniSanaa na Mci hezo.
09/02/2018

IMG-20180209-WA0034.jpg
 
Back
Top Bottom