Ngurubhe
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 1,840
- 1,049
Katika hali ya kawaida metch ya jana haikuwa nzuri kuanzia maandalizi ya pale mlangoni na wapuliza vipenga.
Ilikuwa kama watu walikurupushwa hivyo wakawa wanatakiwa wafanye tu yapite wakati haikuwa hivyo.
Ukiangalia kadi zote zilikuwa zinatoa taarifa ya kuwa ni feki ilihali zimeuzwa na mamlaka husika.Lazkini pia mim najiuliza kama ni tatizo la MTANDAO kama wahuska walivyodai,je hawakufanya prior analysis( testing) ya matumizi ya kadi na hata kuja na alternative kama tu tatizo kama la jana lingrletokea?
Au ndio ule utamaduni wetu wa kufanya betting game kwenye matukio mhimu.
Ukija upande wa wapuliza vipenga,mim najiuliza je huyu referee alikuwa hana mawasiliano na wasaidizi wake wa pemben mwa uwanja?..kama kosa lake ndio liliopelekea watu kuanza kuvunja vitu na hata kusababisha almost hasara zaidi ya M300.je kwanin waziri mwenye dhamana asijihudhuru?
Kama unaweza toa maoni unadhani kwanin hatakiwi kuwajibika,nasema hivi kwa sababu nineona kuna hali ya uzembe kuanzia hukohuko wizarani kwani mashabiki hawa wanaonekana walitoka wanahasira toka huko nje ya uwanja,ukizngatia wengine waliumia hasa baada ya vurugu zilizotokana na milango kuwa haifunguki ilihali wamelipia.