Waziri Mwigulu Nchemba hapa tunapata tumaini

SOEN

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2023
Posts
407
Reaction score
183
Jana, Machi 13 nilipata wasaa wa kusoma hotuba ya Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Mwaka 2022/23, na Vipaumbele vya Kibajeti kwa mwaka ujao wa fedha mbele ya Wabunge Jijini Dodoma.

Chini ya Uongozi bora wa Rais Samia Suluhu Hassan, nchi yetu imepiga hatua kubwa katika kuhakikisha mahitaji ya wananchi yanapewa kipaumbele cha kwanza na kukuza uchumi endelevu.

Tunatarajia kuwa bajeti ya mwaka ujao wa fedha 2023/24, itakuwa takribani Tsh 44.39 trilioni, kwa ajili ya kuendeleza Maendeleo yaliyojikita kwa watu na kukuza uchumi wa Viwanda, ambayo ndio dhima yetu.

Serikali inaendelea kufanya jitihada ili kupata mustakabali bora kwa Watanzania wote.

Tunajitahidi kusaidia na kuweka Mipango ambayo inatanguliza mbele mahitaji ya wananchi wote, kuanzia kwenye miundombinu hadi kuongeza ufikiaji na upatikanaji wa elimu ya viwango na huduma bora za Afya.

Kupitia Uongozi mzuri na mwelekeo sahihi wa Rais Samia Suluhu Hassan, na usimamizi mahiri wa Sera za Uchumi na Fedha, tunaendelea kuunda Tanzania bora, yenye uchumi imara, na inayofaa kwa kila mtu.

Sisi watanzania kwa Umoja wetu, tuendelee kufanya kazi kwa bidii ili kufikia ndoto ya Mheshimiwa Rais.

Kazi Iendelee.
 
Tokea Mama aseme huwa anapita jf kumekua na mabadiliko makubwa sana.
 
Pitia hotuba nzima inajieleza
 
Lema akisoma ataelewa bilashaka
 
Ndiyo lazima ajue mapokeo yetu kama wananchi binafsi nampongeza Mh Mwigulu Nchemba sijaona kasoro
 
Jana, Machi 13 nilipata wasaa wa kusoma hotuba ya Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Mwaka 2022/23, na Vipaumbele vya Kibajeti kwa mwaka ujao wa fedha mbele ya Wabunge Jijini Dodoma.

Chini ya Uongozi bora wa Rais Samia Suluhu Hassan, nchi yetu imepiga hatua kubwa katika kuhakikisha mahitaji ya wananchi yanapewa kipaumbele cha kwanza na kukuza uchumi endelevu.

Tunatarajia kuwa bajeti ya mwaka ujao wa fedha 2023/24, itakuwa takribani Tsh 44.39 trilioni, kwa ajili ya kuendeleza Maendeleo yaliyojikita kwa watu na kukuza uchumi wa Viwanda, ambayo ndio dhima yetu.

Serikali inaendelea kufanya jitihada ili kupata mustakabali bora kwa Watanzania wote.

Tunajitahidi kusaidia na kuweka Mipango ambayo inatanguliza mbele mahitaji ya wananchi wote, kuanzia kwenye miundombinu hadi kuongeza ufikiaji na upatikanaji wa elimu ya viwango na huduma bora za Afya.

Kupitia Uongozi mzuri na mwelekeo sahihi wa Rais Samia Suluhu Hassan, na usimamizi mahiri wa Sera za Uchumi na Fedha, tunaendelea kuunda Tanzania bora, yenye uchumi imara, na inayofaa kwa kila mtu.

Sisi watanzania kwa Umoja wetu, tuendelee kufanya kazi kwa bidii ili kufikia ndoto ya Mheshimiwa Rais.

Kazi Iendelee.
mm nilidhani unashusha nondo kumbe ni bla bla!
 
Pitia hotuba nzima inajieleza
Sehemu ya hotuba ya waziri wa fedha inaonesha kuwa hakuna mradi mpya, maana mfano viwanda vya aina gani tofauti na vile vya waziri Charles Mwijage
"Ukiwa na vyerehani vinne, hicho ni kiwanda kidogo" - Charles Mwijage (Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji) Toa maoni yako
Ukurasa wa 27

4.0 MAPENDEKEZO YA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA WA
MWAKA 2023/24

33. Mheshimiwa Spika, Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa
wa Mwaka 2023/24 yatajielekeza katika kukamilisha utekelezaji wa miradi na programu za maendeleo zilizoainishwa katika maeneo matano ya kipaumbele ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021 / 22 - 2025 / 26).

Maeneo hayo ni:
(i) Kuchochea Uchumi Shindani na Shirikishi: Eneo hili litajikita katika
kuimarisha utulivu wa uchumi jumla; kuboresha uzalishaji na kuimarisha
miundombinu ya usafiri na usafirishaji, umeme na TEHAMA;

(ii) Kuimarisha Uwezo wa Uzalishaji Viwandani na Utoaji Huduma:
Eneo hili litajikita katika kuwezesha ujenzi wa viwanda vinavyotumia
malighafi na rasilimali zinazopatikana nchini; na kuendelea kuboresha
miundombinu ya umwagiliaji, uhifadhi wa mazao, masoko, mifugo na
uvuvi; ikiwemo kuwezesha wananchi kushiriki katika uzalishaji na
kuongeza thamani ya bidhaa hasa zile za kilimo kupitia viwanda vidogo
vidogo.

(iii) Kukuza Biashara na Uwekezaji: Eneo hili litajikita katika kusimamia
utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na
mifumo ya uratibu na usimamizi wa masuala ya uwekezaji, biashara na
masoko;

(iv) Kuchochea Maendeleo ya Watu: Eneo hili litajikita katika kuimarisha
utoaji wa huduma za jamii ikiwemo afya, maji, elimu, utambuzi,
upangaji, upimaji na urasimishaji wa ardhi nchini; na kuimarisha huduma za maendeleo ya jamii na makundi maalumu; na

(v) Kuendeleza Rasilimali Watu: Eneo hili litajikita katika kukuza ujuzi
kwa vijana, kurasimisha ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa
mafunzo; na kutoa mafunzo kwa vitendo mahali pa kazi kwa wahitimu
wa elimu ya juu.

34. Mheshimiwa Spika, Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa
wa Mwaka 2023/24 yataendelea na ukamilishaji wa miradi ya kielelezo yenye matokeo makubwa katika ukuaji wa uchumi inayojumuisha:

Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR);

Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa
Julius Nyerere – MW 2,115;

Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL);

Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga
(Tanzania);

Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia kuwa Kimiminika
(LNG) – Lindi;

na Ujenzi wa Madaraja Makubwa na Barabara za Juu mfano Daraja la Kigongo - Busisi (Mwanza).
 
Jana, Machi 13 nilipata wasaa wa kusoma hotuba ya Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Mwaka 2022/23, na Vipaumbele vya Kibajeti kwa mwaka ujao wa fedha mbele ya Wabunge Jijini Dodoma.

Chini ya Uongozi bora wa Rais Samia Suluhu Hassan, nchi yetu imepiga hatua kubwa katika kuhakikisha mahitaji ya wananchi yanapewa kipaumbele cha kwanza na kukuza uchumi endelevu.

Tunatarajia kuwa bajeti ya mwaka ujao wa fedha 2023/24, itakuwa takribani Tsh 44.39 trilioni, kwa ajili ya kuendeleza Maendeleo yaliyojikita kwa watu na kukuza uchumi wa Viwanda, ambayo ndio dhima yetu.

Serikali inaendelea kufanya jitihada ili kupata mustakabali bora kwa Watanzania wote.

Tunajitahidi kusaidia na kuweka Mipango ambayo inatanguliza mbele mahitaji ya wananchi wote, kuanzia kwenye miundombinu hadi kuongeza ufikiaji na upatikanaji wa elimu ya viwango na huduma bora za Afya.

Kupitia Uongozi mzuri na mwelekeo sahihi wa Rais Samia Suluhu Hassan, na usimamizi mahiri wa Sera za Uchumi na Fedha, tunaendelea kuunda Tanzania bora, yenye uchumi imara, na inayofaa kwa kila mtu.

Sisi watanzania kwa Umoja wetu, tuendelee kufanya kazi kwa bidii ili kufikia ndoto ya Mheshimiwa Rais.

Kazi Iendelee.
Porojo tu
 
Back
Top Bottom