Waziri Mwigulu, tunakupuuza wewe na si Nipashe

Waziri Mwigulu, tunakupuuza wewe na si Nipashe

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
MWIGULU TUNAKUPUUZA WEWE SIYO NIPASHE.

Mwigulu Nchemba, lawama zako usiwape NIPASHE. Umenukuu POST yangu. Sisi ni wamiliki wa pesa zilizopo (BoT). Tunahitaji ufafanuzi wa kueleweka.

NIPASHE wamerejea. (1) ripoti za uwajibikaji 2022/23 zilizotokana na Ripoti za CAG uliofanywa na WAJIBU (2) ukaguzi wa CAG Hesabu za Serikali Kuu 2022/23.

2022/23 serikali iliidhinishiwa Sh. trilioni 41.480. Ukaguzi wa CAG Serikali Kuu 2022/23, umebaini serikali ilikusanya Sh. trilioni 41.880, ziada ya Sh. bilioni 400.

Kati ya Sh. trilioni 41.880 zilizokusanywa, Sh. trilioni 38.447 zilipokewa Mfuko Mkuu wa Hazina, tofauti ya Sh. trilioni 3.4334. Mjadala unaanzia eneo hilo.

Licha ya Serikali kukusanya trilioni 38.447 zilizopita Mfuko Mkuu, (BoT) iliipa (serikali) Sh. trilioni 40.18, hivyo (BoT) kuipa serikali Sh. trilioni 1.7 za ziada.

Kati ya Sh. trilioni 3.433 ambazo hazikupita Mfuko Mkuu wa Hazina 2022/2023, Sh. trilioni 3.197 zilipelekwa moja kwa moja kwenye miradi, ameeleza CAG.

Tofauti inatokana na Sh. trilioni 3.656 zilizopelekwa miradi kutoka wadau wa na makusanyo yaliyopelekwa Zanzibar hayapitii Mfuko Mkuu wa Hazina.

Sh. bilioni 223 zinazotokana na bakaa za makusanyo ya kodi za 2021/22 na makusanyo mengine yaliyopokewa Mfuko Mkuu wa Hazina ya nje ya makisio ya bajeti.

Jumla ya matumizi yaliyofanywa Mfuko kugharamia matumizi ya kawaida na maendeleo 2022/23 ni Sh. trilioni 39.523 bila kujumuisha Sh. bilioni 665.80

Ni fedha zilizorejeshwa (refunds) na matumizi mengine kwenye makusanyo ya Sh. trilioni 38.447, kusababisha nakisi ya Sh. trilioni 1.742 kufikia 30/06/2023

Waziri wa Fedha, unasema Sheria ya BoT inaruhusu kutoa advances or short term loans kwa Serikali kukidhi mahitaji ya matumizi ambayo hayajapata mapato.

Kwanini hiki kitu ambacho Wizara ya Fedha mnakiita mkopo (imegeuka kuwa treasury bond), ambalo ni deni la muda mrefu ambalo Serikali inalipa na riba?

Kwanini mkopo umejumuishwa katika deni la taifa? Mkopo uliotakiwa kuwa wa muda mfupi (short-term loan) kawaida muda wake ni maximum miezi (12)

Kwamba katika miezi hiyo 13 deni lote liwe limelipwa. Tangu Serikali mmechukua fedha hizo kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT)ni miaka miwili sasa imepita.

Lengo la mkopo ni kufidia ‘temporary budget shortfall’ serikali ikipata makusanyo irejeshe mkopo huo. Miaka miwili imepita bado pesa hizo hazijarudi BoT.

Mmehamishia kuwa long-term debt; huo ndio uchotaji wenyewe wa akiba kutoka BoT ambao unaelezwa na utafiti wa WAJIBU kutoka katika taarifa ya CAG.

Temporary shortfalls often occur in response to an unexpected event. Unexpected event gani imetokea iliyowalazimu kuchukua Sh. Trilioni 1.7 kutoka BoT?

Kama makusanyo ya Serikali yalivuka malengo, Serikali imechukua advance loan ya nini BoT? Hizi cash outflows BOT ndiyo zinaendesha hizi timu zenu za IHEFU?

Ripoti za uwajibikaji 2022/23 zilizotokana na uchambuzi wa Ripoti za CAG uliofanywa na WAJIBU umefanywa na taasisi ya WAJIBU siyo maoni ya Mr. Ludovick Utoh.

Mwigulu, usidogodeshe hoja. Watanzania wanahitaji usalama wa fedha zao, siyo porojo. Serikali inakuwa reactive badala ya kuwa proactive. Hakuna uwazi.

Tunahitaji kampuni ya ukaguzi (Auditing firm) kutoka nje kuchunguza UFISADI huu, hatuwezi kupuuza kirahisi tu kwa kuwa tu amesema Mwigulu. Huaminiki.

Kitabu cha MY LIFE, MY PURPOSE, Benjamin MKAPA anajuta kushawishiwa na kamati kuu CCM kutumia Sh230bn za EPA kufadhili kampeni za CCM 2005

Martin Maranja Masese, MMM

Pia soma: Puuzeni taarifa ya Nipashe, hakuna uchotaji fedha BoT
 
Mwigulu ni fisadi asiyestahili kuaminiwa kwenye ufafanuzi wowote anaotoa, mahali popote, ni muongo anayejua anatudanganya ndio maana huogopa kujibu maswali yetu kwa kuogopa kuumbuliwa.

Hii ndio sababu inayomfanya mwingine ajiite chura kiziwi, anajua hana majibu ya uchafu wanaotufanyia watanganyika.
 
Tatizo wanadhani watanzania wa leo ni sawa na watanzania miaka ile ya 90
Kwa kusema vile tu basi imetosha kutolea ufafanuzi wa kukidhi haja.
 
Mwigulu muoga sana hata kujibu hoja kwa mada aliyoanzisha mwenyewe hawezi
 
Mama na hii Timu Wahuni wanainajisi nchi
Naamini wanamtisha sana na yeye anaingia mkenge, huku wakimlambisha na kumuambia Tulia Kila kitu hiko sawa.
Asichokijua atakuja acha legacy mbaya sana.
Maana hao wanao mdhahuri awakumbukwi atakubukwa yeye kama WA awamu yake.
 
Key Features of developed country includes the following characteristics:-

1) High Per Capita Income

2) Diverse industrial mix, including a large services sector

3) Developed financial system

4) Longer life expectancy at birth

5) Well developed educational system.

6) Strong MSME Base
 
Back
Top Bottom