Pre GE2025 Waziri Nape, kutukosesha mtandao wa ClubHouse nchi nzima sababu ya watu wachache ndio upeo wako ulipoishia?

Pre GE2025 Waziri Nape, kutukosesha mtandao wa ClubHouse nchi nzima sababu ya watu wachache ndio upeo wako ulipoishia?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
593
Reaction score
1,376
Wakuu,

Mtando wa ClubHouse umezuiwa kupatika nchini toka mwaka jana (2023) mwanzoni, ambapo huwezi kupata kupata huo mpakata utumie VPN.

Hii ni ukiukwaji wa haki ya kujieleza na kupata kupata habari, ni kwenda kinyume na Katiba ya Tanzania inayotoa haki ya mtu kuwasiliana na kupata habari bila kujali mipaka ya nchi.

Kifupi ni kwamba tuna haki ya kupata mitandao yote iwe ClubHouse, X, TikTok, Instagram, FB, nk kwa mujibu wa Katiba, na anayekwenda kinyume na hili anavunja Katiba na anatakiwa kuchukuliwa hatua.

Watanzania wote tumefanya kosa gani mpaka tuzuiwe mtandao wa ClubHouse? Tumekiuka sheria gani mpaka wote tuzuiwe kutumia mtandao huu? Watu karibia milioni 40 sasa hivi tunakosa mtandao huu sababu "unashughulikia" watu wachache waliovunja sheria? Unaona ni sawa kabisa, na uko proud kama Waziri kufanya ujinga huu?

Waziri Nape ni ipi justification ya wewe kufanya uvunjifu huu wa Katiba?

Unaweza kuja na kisingizio kuna watu wanatumia vibaya mtandao huo kuharibu maadili... wamevunja sheria... sasa kwanini hujawashataki wakawajibika na sisi tukajua uvunjufu huo wa sheria uliofanywa?

Yaani kikundi cha watu wachache ndio kinafanya uzuie mtandao kupatikana nchi nzima? Hapo ndio umefikiria mpaka mwisho ukaona hii ndio suluhu mujaribu ya kutatua changamoto hiyo.

Na tuseme ukweli, "Kwenda kinyume na maadili", au "Kuvunja Sheria" kwa serikali inamaanisha watu wao wamekosoa serikali hivyo wanatakiwa kudhibitiwa.

Kama uwezo ni mdogo si utafute washauri wataalamu kwenye mambo haya wakueleze ukifanya hivi unaleta athari gani na inamaanisha nini kwa Wanzania na nafasi uliyoshika?!

Kusema ukweli wewe Nape kama Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ni MZIGO kwa Taifa na AIBU kwa Rais. Hutoshei kabisa kwenye hiyo nafasi, viatu vinapwaya mno!
 
Unapatikana, labda huna bando au hujui jinsi ya kujiunga na mtandao huo, hata jana nilikuwa clubhouse
 
Moja ya sifa ya watu wasio na uwezo wa uongozi ni pamoja na kuzuia wenye mawazo mazuri na upeo na ufahamu kufanya lolote ili kuleta mabadiliko sababu wanajua hawana uwezo wa kuleta hayo mabadiliko.

Huu anaofanya Nape ni uhuni na ni kuvunja miiko ya utumishi wa uma.
 
Back
Top Bottom