kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,875
Wasalaam wana bodi!
Ndg zangu nimesikitishwa sana na ukimya wa waziri wa sanaa, utamaduni ,michezo na burudani ndg Nape Mnauye kwa kutokuona jinsi lugha adhimu ya kiswahili kinavyoharibiwa na watanzania. Si vyombo vya habari,si wasanii, si raia wa kawaida wala viongozi wakuu katika nchi wote kwa pamoja tumeamua kukiua kiswahili mchana kweupe. Ukifungua radio kuanzia asubuhi mpaka jioni utashangaa jinsi ambavyo kiswahili kinaharibiwa, utasikia wimbo ukiitwa MWIMBO au NYIMBO ikitumika kama umoja wa neno wimbo (Utasikia naomba ile nyimbo ya mdogomdogo wa diamond). Si hayo tu yapo mambo anuai yanayotumiwa na watangazaji na wasanii yanayoharibu lugha ya kiswahili.
Ukirudi kwa waheshimiwa wabunge nako ni shida, kiswahili kinachanganywa na kiingereza bila mpangilio. Yaani mtu kiingereza hakijui lakini utasikia because, so , so that, you know, absolutely, not only but also kibao kwenye sentensi za kiswahili. Hata wakuu wa serikali nao badala ya kuonesha mfano nao pia wameng'ang'ana na kiswaenglish bila sababu za msingi. Utakuta kiongozi anaongea kwa kiswahili huku mkalimani akitafsiri kwa kiingereza na bado anaingiza maneno ya kiingereza kwenye kiswahili sasa kwanini awepo mtu wa kutafsiri? kwanini basi asizungumze tu hicho kiingereza mpaka mwisho?
Tukiendelea hivi kuna kizazi hakitajua kiswahili sanifu wala kiingereza, watakuja na lugha chotara ya kiswahili ,english na lugha za makabila. Waziri Nape kiswahili ni utamaduni wa mtanzania, wizara yako inapaswa kuilinda na kuitetea kiswahili. Peleka muswada bungeni wa kudhibiti watangazaji na vyombo vya habari zinazotumia vibaya lugha ya kiswahili. Na kuweka marufuku kwa viongozi wa umma na wa kijamii kuchanganya kiswahili na kiingereza ili aamua kutumia lugha moja wapo. Bila hatua za makusudi hii lugha itapotea na tutaanza kuzungumza vitu visivyoeleweka kabisa.
NAWASILISHA.
cc, TUKI
cc, BAKITA
cc, BASATA
cc, TCRA