Waziri Nape: Wazazi msiwaache watoto wenu walelewe na mitandao na teknolojia, waleeni ninyi wenyewe taifa linaangamia!

Waziri Nape: Wazazi msiwaache watoto wenu walelewe na mitandao na teknolojia, waleeni ninyi wenyewe taifa linaangamia!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri wa TEHAMA Mh. Nape amewasihi wazazi wa KKKT Kijitonyama, kuwalea watoto wao wenyewe na wasiwaache walelewe na mitandao na teknolojia kwani hali ya kimaadili kwa sasa ni mbaya.

Nape ambaye aliongozana na Waziri wa Fedha Dr Mwigullu Kanisani hapo kwa mchungaji kiongozi Dr Kimaro, amesema yeye kama waziri anajua mitandao ina faida lakini ina hasara kubwa pia. Awali mchungaji Kimaro alisema Nape ni rafiki yake wa muda mrefu na amekuwa akimuombea kwa Mungu wa mbinguni katika mapito yake.

Chanzo: EK tv
 
Inashangaza waziri wa teknolojia kutoa marufuku ya watoto kujikita katika teknolojia.

Ningetarajia awasihi wazazi waingize watoto wao katika fursa ya teknolojia

Kama kuna makosa kwenye teknojia itakayowaathiri watoto , ndiyo mwanzo wa kujifunza
 
Wakati mnawakeep busy wazazi watafute pesa za Tozo msiwalaumu kwa kushindwa kutulia na familia majumbani.

Shame on you Nape and Co
 
Hawa wachungaji Kondoo wa siku hizi wamekuwa wapiga deal tu. Africa tu ndiyo utakuta ujinga kama huu unaendelea makanisani!
 
Waziri wa TEHAMA Mh. Nape amewasihi wazazi wa KKKT Kijitonyama, kuwalea watoto wao wenyewe na wasiwaache walelewe na mitandao na teknolojia kwani hali ya kimaadili kwa sasa ni mbaya
Elimu itolewe kwa mifano, kwanini hakumtolea mfano mtoto wa jamaa yake aliyesumbua traffic police majuzi kama kielelezo
 
Di i zimekuwa kichaka cha watu kutaka waonewe huruma
 
Back
Top Bottom