Waziri Ndejembi Ataka Watendaji Ardhi Kuondoa Urasimu na Kutoa Hati kwa Wakati

Joined
May 14, 2024
Posts
94
Reaction score
75
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Deogratius Ndejembi amewataka Menejimenti na watumishi wa Wizara ya Ardhi kuondoa urasimu na kutoa hati milki za ardhi kwa wakati.

“Tuondoe urasimu, kama mtu ana nyaraka zote zinazohitajika, tuwape hati zao na tukumbuke sisi ni watoa huduma kwa wananchi n ani wizara wezeshi, hati zitolewe kwa wakati na hati zilizotayari wananchi wajulishwe waje wachukue hati zao” amesema Mhe. Ndejembi.

Mhe. Ndejembi amesema hayo Julai 27, 2024 wakati wa kikao na wajumbe wa Menejimenti ya Wizara hiyo mara baada ya kupokelewa Makao Makuu ya Wizara yaliyopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Amewataka watendaji wa sekta ya ardhi nchini kufanya kazi kwa weledi na kusimamia vizuri mifumo ya TEHAMA na Mawasiliano ili wananchi wapate haki yao katika sekta ya ardhi.

“Sijaja kutengua kazi mnazoendelea kuzifanya, nimekuja kuongeza nguvu. Tuzidi kufanya kazi vizuri na kuhakikisha mifumo yetu ya kiwizara kuanzia wilaya, mikoa na wizara ifanye kazi vizuri. Ni vizuri tusimamie haki ya wananchi na mifumo ifanye kazi yake kutoa haki,” amesema Waziri Ndejembi.

Aidha, ameendelea kusisitiza kuendelea kwa Klinik za Ardhi ambapo amesema kasi katika klinik hizo lazima iongezwe kwa kuwa wakati mwingine wananchi inakuwa vigumu kuwafikia makamisha wa ardhi wasaidizi wa mikoa.

Akimkaribisha Waziri Ndejembi kwenye kikao na Menejimenti ya Wizara hiyo, Naibu Waziri Geofrey Pinda amesema Wizara hiyo ina ofisi katika halmashauri zote nchini na kumhakikishia ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake ili kuwahudumia wananchi katika sekta ya Ardhi.

Awali Katibu Mkuu Mhandisi Anthony Sanga akimkaribisha Waziri wa Ardhi wizarani amemuelezea muundo wa wizara na kuainisha idara na vitengo vya wizara hiyo sambamba na taassisi zilizo chini ya wizara hiyo.
 
Utaratibu ulitakiwa uanzishwe na serikali kwa kulazimisha miji ipangwe, waliojenga sehemu ambazo hazijapangwa waondolewe papangwe wapewe bure waendelee na maisha.
 
Anajisumbua tu, Ardhi ni pagumu sana, akiwa legelege huyo Waziri kamwe hawezi kutoboa.

Na kwa bahati mbaya zaidi katika nchi hii, matapeli wa ardhi wengi sana ambao wanaisumbua nchi au hata hao Watumishi wa Wizara ya Ardhi ambao wanaonekana kuwa wasumbufu kwenye suala la utoaji wa huduma kwa Wananchi, wengi wao Wana back-up ya wakubwa huko juu, hata yeye Waziri wa Ardhi hana ubavu wa kuwagusa.
 
Yaan katika sehemu mnatidhoofisha ni Ardhi nina madai ya fidia tokea mwaka 2015 mpaka leo hamjafidia...Ardhi mliichukua pale mkoani Iringa eneo la Igumbilo, na sisi kama wamiliki wa mashamba kipindi hicho, tukiwa ndani ya mradi..eneo lile likawa stand kuu ya mabasi na baadhi ya maaneo mkawamilikisha wananchi baadhi mkawalipa fidia na wengine hamkuwapa nikiwemo mimi na ndan ya eneo langu bahati nzur nilijenga kanyumba kwa ajili ya maswala ya kuhifadhia nafaka ni kweli hapajaguswa.

Alikuja makonda Iringa kipindi akiwa mwenezi nikafunga nae safari akatoa maelekezo kero zishughulikiwe na baadhi ya watumishi waliokaa zaid ya miaka 4, wahamishwe ni kweli akiwemo shirima ambaye alihudumu kwa miaka 10 na ndie mtia sain kipindi cha mchakato wa mwaka 2015 kweli amehamishwa, nilifanya mawasiliano na watumishi wa ardhi kwa ajil ya fidia nikaambiwa nisubiri budget ipite.

Kweli nimesubiri mpaka budget ya mwaka huu imepita, nikawasiliana nao jibu nililopewa wananiambia na wenyewe jambo hili lipo nje ya uwezo wao, labda niende kwa mkurugenzi kwa kweli muda sina. Naombeni mkalishughulikie hili na mkitaka mawasiliano yangu nitawapa documents zote za fidia zipo wazi na mahakamani sitaenda.
 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Deogratius Ndejembi amewataka Menejimenti na watumishi wa Wizara ya Ardhi kuondoa urasimu na kutoa hati milki za ardhi kwa wakati.

“Tuondoe urasimu, kama mtu ana nyaraka zote zinazohitajika, tuwape hati zao na tukumbuke sisi ni watoa huduma kwa wananchi n ani wizara wezeshi, hati zitolewe kwa wakati na hati zilizotayari wananchi wajulishwe waje wachukue hati zao” amesema Mhe. Ndejembi.

Mhe. Ndejembi amesema hayo Julai 27, 2024 wakati wa kikao na wajumbe wa Menejimenti ya Wizara hiyo mara baada ya kupokelewa Makao Makuu ya Wizara yaliyopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Amewataka watendaji wa sekta ya ardhi nchini kufanya kazi kwa weledi na kusimamia vizuri mifumo ya TEHAMA na Mawasiliano ili wananchi wapate haki yao katika sekta ya ardhi.

“Sijaja kutengua kazi mnazoendelea kuzifanya, nimekuja kuongeza nguvu. Tuzidi kufanya kazi vizuri na kuhakikisha mifumo yetu ya kiwizara kuanzia wilaya, mikoa na wizara ifanye kazi vizuri. Ni vizuri tusimamie haki ya wananchi na mifumo ifanye kazi yake kutoa haki,” amesema Waziri Ndejembi.

Aidha, ameendelea kusisitiza kuendelea kwa Klinik za Ardhi ambapo amesema kasi katika klinik hizo lazima iongezwe kwa kuwa wakati mwingine wananchi inakuwa vigumu kuwafikia makamisha wa ardhi wasaidizi wa mikoa.

Akimkaribisha Waziri Ndejembi kwenye kikao na Menejimenti ya Wizara hiyo, Naibu Waziri Geofrey Pinda amesema Wizara hiyo ina ofisi katika halmashauri zote nchini na kumhakikishia ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake ili kuwahudumia wananchi katika sekta ya Ardhi.

Awali Katibu Mkuu Mhandisi Anthony Sanga akimkaribisha Waziri wa Ardhi wizarani amemuelezea muundo wa wizara na kuainisha idara na vitengo vya wizara hiyo sambamba na taassisi zilizo chini ya wizara hiyo.
Matatizo hayaondolewi kwa ''kutaka''. Hawa CCM wote ni vilaza? Matatizo yanaondolewa kwa matendo.
 
Ni jambo jema kama mmeamua kuwasogelea wananchi kupitia mitandao .

Watanzania tumechoka na matamko , tunahitaji vitendo zaidi .

Kero zinazohisu ardhi ni Nyingi sana zinahitaji utatuzi wa haraka , watu wasikae kwenye migogoro muda mrefu wengine mpaka wanakufa migogoro yao ya ardhi bado haitatiliwa hili linakuwa halijakaa sawa .

Kikubwa tunahitaji vitendo matamko yashakuwa mengi sana .​
 
Back
Top Bottom