Wizara ya Ardhi
Member
- May 14, 2024
- 94
- 75
"Nafahamu mgogoro huu umedumu kwa muda mrefu lakini niwahakikishie hakuna kisichowezekana, ni lazima kupata suluhu. Hivyo nimtake Mwekezaji wa Shamba hili la Malonje kutoendeleza upandaji wa mazao ya kudumu lakini pia na wananchi msiingilie shamba hili hadi suluhu itakapopatikana.
Lakini pia nimuelekeze Kamishna wa Ardhi kutuma timu ya wataalamu kutoka Wizarani kuja hapa Sikaungu kupitia upya mipaka yote ya shamba hili na kuona ukubwa wake na uhalisia wa vipimo vilivyopo, kazi hii ifanyike ndani ya siku 14 ili tuweze kupata ufumbuzi wa jambo hili mapema,” Ameelekeza Mhe. Ndejembi.
Katika ziara hiyo, Mhe Waziri Ndejembi ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mhe. Nyakia Chirukile pamoja na timu ga wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiwemo, Kamishna wa Ardhi Bw. Mathew Nkhonge.