Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Waziri wa Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Oktoba 15, 2024 Manispaa ya Songea ameendelea na zoezi la kuhamasisha wananchi wa manispaa hiyo kujitokeza kwa wingi katika vituo vya uandikishaji kwenye daftari la wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024.
Katika hamasa hiyo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ametumia usafiri wa Bajaji kupita katika mitaa mbalimabli ya manispaa hiyo kuhamasisha wananchi hao huku akiwaeleza umuhimu wa kujiandikisha.
Aidha, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekagua maendeleo ya uandikishaji katika vituo vya uandikishaji ikiwemo, Mashujaa, Ruvuma na Mateka ambapo amesema kuwa zoezi hilo linaendelea vizuri.