LGE2024 Waziri Ndumbaro atumia bajaji kuhimiza wananchi kujiandikisha Daftari la Mpiga Kura Songea

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

Waziri wa Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Oktoba 15, 2024 Manispaa ya Songea ameendelea na zoezi la kuhamasisha wananchi wa manispaa hiyo kujitokeza kwa wingi katika vituo vya uandikishaji kwenye daftari la wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024.


Katika hamasa hiyo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ametumia usafiri wa Bajaji kupita katika mitaa mbalimabli ya manispaa hiyo kuhamasisha wananchi hao huku akiwaeleza umuhimu wa kujiandikisha.


Aidha, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekagua maendeleo ya uandikishaji katika vituo vya uandikishaji ikiwemo, Mashujaa, Ruvuma na Mateka ambapo amesema kuwa zoezi hilo linaendelea vizuri.


Pia soma: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
The comical Ndumbaro.Angeelekeza tu kwenye simu zetu tu-download application yake ya vichekesho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…