Waziri: Njaa kali yafelisha watoto: Dk Kawambwa apata wakati mgumu mbele ya JK

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801

JUMAMOSI, FEBRUARI 23, 2013 04:23 NA MWANDISHI WETU

*Dk Kawambwa apata wakati mgumu mbele ya JK

WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza, amejitosa katika sakata la mitihani na kusema wanafunzi wamefeli kutokana na njaa.

Kauli ya Chiza imekuja wakati ambao, matokeo ya kidato cha nne yaliyotolewa hivi karibuni, yanalalamikiwa kwa sababu ya idadi kubwa ya wanafunzi kufanya vibaya.
Chiza alitoa kauli hiyo jana, mbele ya Rais Jakaya Kikwete katika hafla ya uzinduzi wa utaratibu wa mfumo mpya wa usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo, iliyofanyika katika hoteli ya White Sands Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Chiza alisema suala la uzalishaji wa chakula ni muhimu ili kuondokana na matatizo ya njaa shuleni.

Alisema kilimo ni sekta mtambuko, hivyo haina budi kupewa kipaumbele, kwani inapolega athari yake ni kubwa kijamii na hata kiuchumi.

"Wanafunzi wamefeli mitihani kwa sababu ya njaa, hivyo lazima tuongeze uzalishaji wa mazao ya chakula ili kuondokana na tatizo hili," alisema huku wajumbe wakiangua kicheko ukumbini.

Katika hafla hiyo, Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa alipata wakati mgumu katika mkutano huo.

Kawambwa alikumbwa na hali hiyo baada ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo kucheka kila aliposimama.

Mara ya kwanza, walicheka wakati Rais Kikwete alipokuwa akiwatambulisha Mawaziri na wao kusimama.

Kawambwa alichekwa mara ya pili wakati aliposimama mbele kuelezea suala zima la elimu na changamoto zake kwa wajumbe wa mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na watu wa mataifa ya nje.

Hali hiyo haikumfurahisha Dk Kawambwa, ambapo kabla ya kuzungumza alikaa kipya kidogo kasha kusema.

"Nasononeka sana,mnapocheka najisikia vibaya," alisema Dk Kawambwa kasha kuendelea kueleza juhudi zinazofanywa na wizara yake kuinua elimu nchini.

Kitendo hicho kilimlazimisha Waziri wa Kilimo, Chiza kutafuta namna ya kumnusuru Kawambwa akitumia fursa aliyopewa kuzungumza kwa dakika tatu juu ya sekta ya kilimo mbele ya wajumbe ambao ni watalaamu mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

Chiza badala yake, alianza kwa kusema wakati anakuja kwenye mkutano huo walikuwa wanajadiliana juu ya matatizo ya watoto kufeli mitihani na kugundua kuwa njaa ndiyo kikwazo.

"Watoto wetu hawafaulu kwa sababu ya njaa, na chini ya mfumo huu mpya utakuja na ufumbuzi huo" alisema Chiza ambaye pamoja na mambo mengine alisisitiza kuwa Wizara yake imejidhatiti kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula ifikapo 2015.

Kauli ya Chiza ilitanguliwa na ya Kawambwa ambaye wakati amesimama kuelezea suala zima la elimu mbele ya mkutano huo, alilizamika kueleza wazi kuwa amesononeshwa na kitendo cha kumcheka.

Baada ya kusema hivyo, Kawambwa aliendelea kuzungumza kwa kushukuru suala la elimu kuingizwa kwenye mfumo huo ambao alisema anaamini utakuja na ufumbuzi wa matatizo yanayoikabili sekta hiyo.

Matatizo makubwa yaliyosababisha kidato cha nne kufeli ni upungufu wa walimu wakiwamo wa sayansi, upungufu wa vifaa ambapo alisema, mchakato wa mfumo huo utasaidia kutoa majibu ya hayo yote.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mkutano huo, Kawambwa alisema semina hiyo ni kama imeota imekuja wakati ambapo matokeo ya kidato cha nne yametoka mabaya.

Hata hivyo Kawambwa alisema kufeli kwa wanafunzi kunatokana na sababu kuongezeka kwa udhibiti wa mitihani.

"Udhibiti umekuwa mkubwa safari hii, husikii mahali popote kama mtihani ulivuja…haya ni mafanikio, miaka ya nyuma watu walikuwa wanajiuliza hata huyu kafaulu?" alisema Kawambwa.

Kawambwa aliitaja sababu nyingine kuwa ni kushuka kwa kiwango cha udanganyifu.

"Mwaka jana tuliwafutia matokeo kwa udanganyifu watoto 3330, mwaka huu idadi imepungua, matokeo haya ni ya kweli" alisisitiza Kawambwa.

Alisema pengine wazazi wanaweza kusema shule za sekondari za serikali zimefanya vibaya jambo ambalo alisema si kweli.

Kawambwa alisema hata shule binafsi na seminari pia zimefanya vibaya katika matokeo hayo kutokana na sababu hizo.

Kawambwa alisema jambo hilo si la kufurahia lakini pia si la kuingiza siasa za bei nafuu ambazo hazitaki.

Kwa karibu wiki sasa, Waziri Kawambwa amekuwa akiandamwa, huku baadhi wakimtaka ajiuzulu, kutokana na sekta ya elimu kufanya vibaya.

Hata hivyo jana gazeti hili lilimkariri Kawambwa akisema hawezi kujiuzulu kwa sababu ya wanafunzi kushindwa mitihani na kwamba hiyo ni lugha ya kisiasa.

Kawambwa alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa tatizo si yeye bali ni mfumo wa elimu, hivyo kujiuzulu kwake hakutasaidia lolote.

SOURCE; MTANZANIA

 
huenda ni kweli kwani enzi zetu tulikuwa tunakula viazi maganda na nyama pale Tambaza
 
Nina mpango wa kutaka kusoma PhD, lakini kwa majibu haya ya Mh. Kawambwa naona kama Masters yangu inanitosha. Kwa kweli I'm very disappointed.
 
Hahahahaaaaaaaaaaaaaa! hii ya CHIZA nayo kali watoto wamefeli kwa sababu ya njaaa!? du yaha watanzania kazi kwen bado yatujackia ya tume iliyoundwa leo na waziri mkuu kama imeundwa ili kufunika kombe mwanaharamu apite tutasikia mengi ya ajabu.

Wengi wanasema Shukuru ajiudhuru! lkn mimi nasema MZEE MZIMA JK na chama chake ndo anapashwa kustep down kwa kushindwa kutatua matatizo lukuki yanayoikabili secta ya Elimu nchi ambayo mengine yamechangiwa na sera yao ngumu na ya kukurupuka ya shule za kata. kwani tumeendelea kushuhudia mdororo kila mwaka tangu mzee wetu aingie madarakani huku tukishuhudia kuongezeka kwa matatizo kwa waalimu badala ya kupungua.
 

Ukweli CCM ni janga. Badala ya kutafuta suluhu ya kuondoa janga la kufeli kwa watoto wetu, yamebaki kuteteana eti wanafunzi wamefeli kwa sababu ya njaa. Hivi hii mijitu ina akili za aina gani? Ukienda Bungeni yanateteana, ukienda kwenye mikutano yanateteana, yakiwa hata kwenye semina yanateteana. Yaani hata mkuu wa nchi naye anakubali Mawaziri kucheka wakati hii ni aibu yake??!!! au ndiyo hivyo tena hana MSHIPA WA SONI!!!!

Ukweli ni kwamba, serikali hii haina mpango wa kutatua tatizo la elimu nchini. Kila siku ni sababu za kuteteana badala ya kutafuta ufumbuzi wa janag hili. Kweli CCM ni JANGA.
 
Chizaaaaaaaaa sasa hii njaa kuwa specific wa boarding au hata wale wa DAY?
Mawaziri wa JK full Cinema
 

matatizo katika sekta ya elimu ni makubwa na yanahitaji tafakari pana. si vema pia kumlaumu kawambwa kwani kinachotea kwa sasa ni matokeo ya mfumo mmbovu wa elimu ulioanzishwa na joseph mungai
 
Hao ndio mawaziri wa JK..like father like... they can speak anyhow... Eti watoto wamefeli sababu ya njaa...watoto wamefeli sababu ya kushuka kwa kiwango cha udanganyifu nk. Nasema hivi kama unafundisha watoto 10 wakafeli 9 tatizo kubwa ni anayefundisha hao watoto kwa maana hiyo ni serikali. Kawambwa anasema tatizo ni mfumo...hivi huo mfumo anausimamia nani kama si waziri mwenye dhamana? Kweli kuitwa Dr hakumaanishi kuwa mtu ana uwezo kuelewa maswala semina elekezi kibao lakina wapi!.

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Waziri wa kiliomo,chakula na ushirika,mhandisi Christopher Chiza amesema njaa kali ndio imesababisha kufeli vibaya kwa wanafunzi.

Waziri huyo alitoa kauli hiyo mbele ya raisi Kikwete wakati wa hafla ya uzinduzi wa utaratibu mpya wa usimamizi na udhibiti wa miradi ya maendeleo iliyofanyika jana jiji Dar es salaam katika hotel ya white sands.

Hata hivyo,kauli hio ilisababisha kicheko kuoka kwa washiriki wa hafla hiyo.

Source:Mtanzania online la trh 23/02/2013.
 
Mipango lukuki kila siku govt inaibuka nayo!MKURABITA,MKUKUTA bado tathmini hatujapewa
 
hata wabadili wimbo namna gani, chanzo ni serikali sikivu ya sisiemu wanao ibia wananchi wake kuanzia umeme, mishahara, usafiri ulio bora na kadhalika, sasa hapo chakula kitapatikana wapi. kama maisha bora wameshindwa kuleta na kukuza uchumi.
 
Kwa hiyo ile single ya Utandawazi kuwa ni sababu ya watoto kufeli, imeshachuja?
Kweli viongozi wetu utafikiri wameondolewa ubongo vichwani mwao. Kama mambo ya intenet yangekuwa ni sababu ya kumfelisha mwanafunzi, basi katika nchi zilizoendelea wanafunzi karibu wote wangekuwa wanafeli maana mambo ya mitandao yameanza zamani ukiachilia mbali kila mwanafunzi ana computer yake.
 

Huyu Waziri nahisi ana njaa ya mawazo!
 
matatizo katika sekta ya elimu ni makubwa na yanahitaji tafakari pana. si vema pia kumlaumu kawambwa kwani kinachotea kwa sasa ni matokeo ya mfumo mmbovu wa elimu ulioanzishwa na joseph mungai

Msitake kumsingizia joseph Mungai. Ni miaka mingapi tangu J. Mungai ameondoka kwenye uwaziri wa elimu? Ina maana kipindi chote hicho cha J. Mungai kuondoka serikali ya Kikwete haikuwa na taarifa juu ya ubovu wa elimu kipindi cha Mungai? kama haikuwa na taarifa basi serikali hii haina sababu kuendelea kutawala nchi hii!!!

Kila siku wanakuja na visingizio visivyo isha. Mbona kwenye kampeni za kuomba kura walituahidi kwamba wanayajuwa matatizo ya elimu na kuahidi kuyashughulikia???!!! Leo wakija na sababu za kwamba tatizo ni Mungai tuwaeleweje?

Mara oooh, nani asiyejuwa matatizo ya elimu, oooh nani asiyejuwa matatizo ya maji, na mambo mengine kama hayo. Wakati wanaomba kuongoza, tulikuwa tunayajua yote haya. na wao aliahidi kuyakabili na kuyatatua. Leo hii wakija na ngonjera na mashairi ya akina TOT yasiyo kuwa na vina wala mizania tuwaeleweje kama sio kukosa uhalali wa kuongoza nchi hii???

Kwa vile wanaonekana kushindwa kila kitu, ni vyema wakabwaga manyanga ili wenye uwezo na utashi wa kuongoza habebe majukumu.

Kila mahali ni usanii mtupu. Bungeni na taasisi zingine ubababishaji kibao ikiwa ni pamoja na kulindana. wanatakiwa kutambua kwamba watanganyika wamechoka na ubabaishaji huu.
 
Mipango lukuki kila siku govt inaibuka nayo!MKURABITA,MKUKUTA bado tathmini hatujapewa

Mkuu!

Tathmini ikifanyika unategemea nini Mkuu?

Yaani mtu aimbe wimbo mwenyewe kisha ajipigie makofi mwenyewe, halafu umuulize aliupokeaje wimbo aliouimba (kwamba ulikuwa mzuri au la)!!?? Natumaini jibu unalielewa mkuu!! Tena kwa hawa MAGAMBA waliokosa hata mishipa ya aibu!!!
 
ukiona kobe yupo juu ya mti ujue kuwa kapandishwa na mtu ,kwa kweli huyu waziri Engineer Chiza aache kabisa kuhadaa umma wa watanzania ,Mheshimiwa raisi wetu hawa ndio mawaziri ambao hawakusaidii hata kidogo
 
Serikali ni moja ila mpaka sasa hili ni tamko la 100 kutoka kwa mawaziri kuhusiana na ufaulu wa watoto wa kidato cha 4.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…