ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 631
- 1,577
WAZIRI PINDI CHANA AWAJIBISHWE MARA MOJA – VITENDO VYA UKATILI MAMLAKA ZA HIFADHI DHIDI YA WANANCHI VIMEFIKIA HATUA MBAYA
Msimamo wa ACT Wazalendo kutokana na matukio uvunjifu wa haki za binadamu yalifanywa na Mamlaka za Hifadhi nchini hivi karibu; kuuawa kwa kwa risasi za moto Ndugu. John James (35) Mkazi wa Chanika - Dar es salaam; Kuchomwa na kubomolewa kwa nyumba za wakazi wa eneo la Bondo, Kilindi – Tanga na Kuvamiwa na kuvujwa kwa Makazi katika Vitongoji vya Ijia, Mlimba – Morogoro.
Anthony M. IshikaChama cha ACT Wazalendo kinalaani vikali mwendelezo wa ukatili na unyanyasaji wa wananchi unaofanywa na Mamlaka za Hifadhi nchini yaani- Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Mamlaka ya Wanyama Pori (TAWA), na Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (TANAPA) huku Waziri wa Maliasili na Utalii, Pindi Chana, akishindwa kuchukua hatua stahiki kwa kipindi chote hiko. Matukio haya ni ishara kuwa Serikali ya CCM haijali hata kidogo thamani ya utu na kuendelea kupuuza wazi wazi haki za msingi za wananchi.
Katika kipindi cha wiki moja, tumeshuhudia matukio ya kikatili yasiyovumilika;
I. Kuondolewa kwa Makazi, Kilindi- Tanga
Mnamo Machi 2, 2025, tumeona taarifa za wananchi kutoka Kitongoji cha Bondo, kilindi Tanga waliokuwa wakiishi kwenye ardhi yao kwa zaidi ya miaka 56. Wakionekana wakipaza sauti na kueleza madhila waliyopitia ya kufukuzwa kwa nguvu, nyumba zao takribani 2,600 zikichomwa moto na kubomolewa na kupoteza ardhi yao yenye ukubwa wa hekta 70,300. Operesheni hii imewaacha wananchi zaidi ya 7,000 bila makazi na mashamba.Huu ni unyama wa kiwango cha juu na unakiuka haki za binadamu.
II. Ukatili wa TAWA, Mlimba- Morogoro
Pili, Februari 27, wananchi wa Mlimba, Morogoro, walifukuzwa kwa mazingira yale yale ya kidhalimu, wakiachwa bila makazi wala msaada wowote kutoka kwa serikali. TAWA, imevunja nyumba takribani 136 za wanakijiji katika kijiji cha Ijia kilichopo Kata ya Mchombe, Tarafa ya Mchombe Wilaya ya Kilomberro, Morogoro na kuacha watu 816 bila makazi.
III. Tukio la Mauaji- Kisarawe, Pwani.
Zaidi ya haya, Februari 28, 2025 tumeshuhudia ukatili zaidi baada ya Maafisa wa Misitu kumuua kwa kumpiga risasi ya moto John James (35) mkazi wa Chanika, Dar es salaam. Alipigwa risasi katika paji la uso akiwa katika kitongoji cha Kikwete Kata ya Marumbo Wilayani Kisarawe. Askari wa TFS waliokua na silaha na gari ya TFS walidai kuwa alibeba mkaa, lakini wakati anapigwa risasi hakuwa na mkaa wowote.
ACT Wazalendo inalaani kwa nguvu zote matukio haya! Ni wazi kwamba vyombo vya serikali vimepewa Mamlaka ya kufanya ukatili dhidi ya wananchi, na hakuna anayewajibika. TFS, TAWA, na TANAPA wamejigeuza kuwa vyombo vya dhuluma, na kujiona wapo juu ya sheria, huku Waziri wao akikaa kimya bila kuchukua hatua.
Tunashuhudia mara kadhaa Serikali ikiendesha operesheni za kuwaondoa wananchi kwenye ardhi zao bila fidia au kwa fidia kiduchu tena bila kuwashirikisha au kupata ridhaa zao (free, prior, informed consent). Mara zote zimekuwa zikisababisha uvunjifu wa haki za binadamu unaoacha maumivu, vilio, vifo, majereha ya kudumu, kutia ulemavu, kupotea kwa amani na kusababisha umaskini kwa wananchi.
Ndugu Waandishi wa Habari
Tujiulize hivi Serikali hii inafanya ukatili wote huu mara kwa mara kwa maslahi ya nani, ikiwa wananchi ndio wanaopaswa kunufaika na uwajibikaji na Serikali mbona inapata ujasiri wa kuua wananchi, kusababisha vilema vya kuduma, kusababisha uvunjivu wa utulivu? Mbona inasababisha umasikini na ufukara mkubwa kwa wananchi hao hao inaosema inataka kuwatetea?
Uhifadhi, Utalii na usimamizi wa ardhi nchini haupo kwa ajili ya wananchi wanyonge. Inaonesha namna hoja ya kulinda uhifadhi ilivyojengeka katika mtazamo wa chuki dhidi ya wananchi kwa kuona kuwa hawana uwezo wa kushiriki kwenye uhifadhi wa mazingira yao isipokuwa kuondolewa. Serikali, Mashirika binafsi na Kampuni kubwa za hifadhi ya wanyamapori na misitu yanapanga njama kwa mgongo wa hifadhi sio tu kuondosha kwa nguvu jamii za kienyeji katika ardhi yao – bali pia kuondosha kabisa uwepo wao. Mtazamo huu lazima utokomee.
Ni wazi kuwa matukio haya ni sehemu ya mpango mpana wa serikali ya CCM kuendelea kuwadhulumu wananchi wake, hasa wale wa kipato cha chini. Hakuna nchi inayoweza kuendelea kwa kupora haki za raia wake. Ardhi ni msingi wa maisha ya wengi na wananchi hawawezi kuendelea kunyanyaswa kwa faida ya wachache wenye Mamlaka.
ACT Wazalendo inataka hatua zifuatazo zichukuliwe kwa haraka zaidi kuzuia ukatili, ukandamizaji na dhulma kwa wananchi wa nchi hii:
i. Waziri Pindi Chana ajiuzulu mara moja kwa kushindwa kuzuia vitendo hivi vya ukatili na udhalimu dhidi ya wananchi.
ii. Uchunguzi huru wa haraka ufanyike juu ya matukio haya yote na waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria.
iii. Serikali isimamishe mara moja operesheni zote za dhuluma zinazoendelea dhidi ya wananchi katika maeneo yao ya asili.
iv. Fidia itolewe kwa waathirika wa ukatili huu mara moja na wahakikishiwe kwamba vitendo hivi havitarudiwa.
ACT Wazalendo itaendelea kupigania haki za Watanzania wote, kupinga unyanyasaji huu, na kuhakikisha kuwa serikali inawajibika kwa vitendo vyake. Raia wa Tanzania wanapaswa kuwa na uhakika wa maisha yao bila hofu ya kufukuzwa kwenye ardhi yao au kuuawa kwa mabavu. Hatuwezi kukaa kimya wakati serikali inapuuza maisha ya watu wake!
Imetolewa na;
Ndg. Anthony M. Ishika
Naibu Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii- ACT Wazalendo
04 Machi, 2025
Pia soma:
~ Serikali ingilieni kati Fidia ya Uharibifu wa Mazao yaliyoharibiwa na Tembo Wilayani Ngara - Kagera: Sheria ya Wanyamapori inakandamiza Wakulima
~ Rais Samia: Viwango vya Fidia kwa wanaoathiriwa na uvamizi wa Wanyama viangaliwe
Msimamo wa ACT Wazalendo kutokana na matukio uvunjifu wa haki za binadamu yalifanywa na Mamlaka za Hifadhi nchini hivi karibu; kuuawa kwa kwa risasi za moto Ndugu. John James (35) Mkazi wa Chanika - Dar es salaam; Kuchomwa na kubomolewa kwa nyumba za wakazi wa eneo la Bondo, Kilindi – Tanga na Kuvamiwa na kuvujwa kwa Makazi katika Vitongoji vya Ijia, Mlimba – Morogoro.
Anthony M. Ishika