JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Silaa ameyasema hayo leo Oktoba 15, 2024 wakati akifungua kongamano la nane la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Tanzania, linaloendelea Jijini Dar es Salaam.
"Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. Rais Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuwekeza kwa kasi kubwa katika TEHAMA ambayo ndio nguzo kuu ya kufikia Uchumi wa Kidijitali Duniani, Dunia hivi sasa ipo katika kipindi cha Mapinduzi ya Nne, Tano na Sita ya viwanda ambapo shughuli za kiuchumi, kijamii na uzalishaji kwa kiasi kikubwa inakwenda kuendeshwa kwa kutumia teknolojia za juu za TEHAMA," amesema Silaa.