Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Leo, Jumanne, 1.10.2024, Mhe George Simbachawene, Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ameweka Jiwe la Msingi wa ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) - Jimbo la Musoma Vijijini
Hospital hii imeishaanza kutoa Huduma za Afya.
Serikali inafanya uwekezaji mkubwa kwenye Hospitali hii iliyoko kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijijini Suguti.
Gharama za uwekezaji hadi leo hii ni kama ifuatavyo:
(i) Gharama za ujenzi: Tsh 3.53 bilioni
(ii) Vifaa tiba: zaidi ya Tsh 2.00 bilioni (X-ray, ultrasound, oxygen plant, etc)
SHUKRANI:
CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa imerikodi shukrani kutoka kwa wananchi wa Musoma Vijijini - tafadhali isikilize.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumanne, 1.10.2024