Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
WAZIRI STERGOMENA TAX MSIBANI KUMFARIJI MBUNGE BONIVENTURA KISWAGA
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb), tarehe 1, Julai 2024 ameungana na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza nyumbani kwa Mbunge wa Jimbo la Magu, Mheshimiwa Boniventura Kiswaga, kumfariji kufuatia kifo cha Mjukuu wake, Kiswaga Philip, aliyefariki tarehe 30, Juni 2024, kwa ajali ya pikipiki eneo la Kisesa, Magu, mkoani Mwanza.
Viongozi kutoka Makao Makuu ya Wilaya ya Magu walioungana na Waziri Tax, kumfariji Mbunge Kiswaga, ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya, Bw. Mohamed Ramadhani na Viongozi wengine waandamizi wa Wilaya.