Waziri Ulega hebu acha mikwara, mimi niliwashauri mapema ila wizara yako ikanipuuza

Waziri Ulega hebu acha mikwara, mimi niliwashauri mapema ila wizara yako ikanipuuza

6 Pack

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2022
Posts
2,819
Reaction score
5,996
Niaje waungwana

Mheshimiwa waziri Abdallah Ulega juzi kati alituacha na mshangao mkubwa watanzania, kwa kujifanya anawapiga mkwara mzito wachina wanaojenga barabara zetu za mabasi ya BRT.

Kwa mtu ambae ndio kwanza anafuatilia mambo hayo ya ujenzi wa barabara za BRT, anaweza kumuona waziri Ulega anapambana kweli kweli na wachina hao, lakini kwa sisi ambao tulianzisha mapambano tukapuuzwa na wizara ya waziri huyo basi tunamuona kama vile ni mtu anaefanya siasa na mikwara isiyokuwa na tija yoyote. Na sababu za sisi wengine kumuona kuwa anapiga mikwara ya kisiasa ni hizi hapo chini.

1. Mimi niliwahi kuandika uzi humu JF kuelezea namna jinsi ujenzi huo unavyoenda kwa mwendo wa kono kono, na kuishauri serikali kupitia wizara ya ujenzi kuwawajibisha wasimamizi wa kampuni hiyo inayojenga barabara zetu kwa mwendo wa pole pole na kwa chini mno ya kiwango.

2. Nikashauri kuwa kampuni hiyo inyang'anywe tenda hiyo na kupewa kampuni nyingine zenye uwezo wa kujenga barabara zetu mapema uwezekanavyo ili kufidia muda mchache uliobaki wa kukamilika kwa ujenzi huo.

Bahati mbaya wahusika walisoma na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa mpaka juzi ikiwa ni mwezi mmoja tu umebaki eti ndio wizara inashtuka na kuamua kuchukua hatua ambayo walipaswa kuichukua mapema kipindi kile nilichoshauri.

mpaka sasa takriban miaka miwili sasa inakaribia lakini ujenzi ndo kwanza upo 23% tu. Je mwezi mmoja uliobaki ndo utaweza kumaliza 77% zilizobaki?

Lakini mtu unaweza kujiuliza kwamba miradi hii inajengwa jijini Dar es salaam, tena katika barabara ambazo viongozi wa serikali mkiwemo wa wizara ya ujenzi hua mnapita.

1. Hivi miaka yote miwili hamkuwa mnaona jinsi ujenzi unavyosinzia?

2. Kama mlikuwa mnaona je ni hatua gani mlianza kuchukua ili kuhakikisha uzembe, ujinga na upuuzi wa wanaojenga haujirudii?

Waziri unasema kuwa Tanzania sio shamba la bibi, lakini ujenzi ambao ungeisha kwa mwaka mmoja umechukua miaka miwili bila kufikisha hata robo ya ujenzi. Sasa kusema sisi sio shamba la bibi sijui unamaanisha nini na wakati kama sio shamba la bibi ulipaswa kuchukua hatua hii mapema ili kumaanisha ulichoongea juzi.

Huu upuuzi wanaoufanya wachina nchini kwetu, kamwe hawawezi kuufanya Rwanda au Kenya. Just ni Tanzania tu kwa sababu wanajua kuwa viongozi wetu sio wawajibikaji. Hakuna mwenye uchungu na nchi wala uzembe wa uwajibikaji.

Hata hivyo kama kweli umeamua kuwachukua hatua na kulisimamia swala hilo basi unapaswa ufanye mambo haya ili kuwapushi waweze kumaliza miradi yetu haraka.

1. Kamata hao viongozi wa kampuni uliokuwa unaongea nao siku ile tupa jela, na utoe masharti kwamba hakuna atakaeachiwa mpaka barabara zetu ziishe. Hii itasaidia kupush haraka barabara hizo, ili ndugu zao waweze kuachiwa. Lakini pia itatuma ujumbe kwa kampuni zingine kwamba Tanzania sio shamba la bibi tena au kichwa cha mwendawazimu kila mtu anajifunza kunyolea kwetu au kufanya utumbo kwenye miradi yetu.

2. Najua wale viongozi wao uliosema waje mwezi ujao hawatokuja. Hivyo baada ya kuwatia ndani amri nyingine iwe kulipa fidia kwa kukataa kutii agizo halali la waziri wa ujenzi ambae ndio dereva wa mikataba hiyo ya ujenzi.

Usipochukua hatua kwa hili basi utadharauliwa sana na kuonekana kuwa wewe ni debe tu lisilo na chochote ndani. Lazima tufukie hatua na sisi tuheshimiwe kama zinavyoheshimiwa nchi za Rwanda na Kenya pale zinapotoa tenda za miradi mbali kwa makampuni ya nje. Pia ubora wa barabara upitiwe upya ili kuangalia kama kuna sehemu wamelipua lipua tu ili mradi uende matokeo yake baada ya mwaka mmoja barabara zinaanza kuwa na mashimo Kibao. Lakini pia nashauri uongozi wa Tanroad na Tarura uchunguzwe. Ni kama kuna sehemu hapako sawa.

Moderators naomba mniwekee huu uzi hapo chini maana mimi nimejaribu imeshindikana
 

Attachments

  • Screenshot_20250313-181629.jpg
    Screenshot_20250313-181629.jpg
    258.8 KB · Views: 2
Naam mhe. Ulega umeuona ujumbe wako?
 
Back
Top Bottom