Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema katika utendaji wake asitarajiwe kuonekana zaidi ofisini bali atajikita kwenye ziara kukagua miradi mbalimbali ikiwemo barabara, ili kuona uhalisia wa utekelezaji wake.
Amesema Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya uboreshaji na ujenzi wa miundombinu hivyo, lazima afuatilie kwa ukaribu kujua utekelezaji wake hasa kwa kuzingatia viwango na ubora uliowekwa.
Ulega ameeleza hayo leo Ijumaa Januari 10, 2025, alipokuwa akizungumza na wananchi wa Njia Nne wilayani Kilwa mkoani Lindi, muda mfupi baada ya kukagua ujenzi wa daraja la Mikerenge'nde ambalo liliathiriwa na mvua mwaka 2024.
"Niwahakikishie nitakuwa mkaguzi kila mara, siyo wa kusimuliwa na kuandikiwa kwenye madaftari nitakwenda mwenyewe kujua kinachoendelea," amesema Ulega.