Waziri Ulega: Tunafanya kazi usiku na mchana kulinda amani

Waziri Ulega: Tunafanya kazi usiku na mchana kulinda amani

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Waziri wa Ujenzi na mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega ameaungana na wananchi wa wilaya hiyo, kufanya dua maalumu ya kumuombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa majukumu yake, pamoja na kuliombea Taifa ili liwe na amani, umoja na mshikamano utakaowezesha maendeleo endelevu.

Dua hiyo imefanyika jana Jumamosi katika uwanja wa Shule Msingi Mkuranga mkoani Pwani ambapo ilihudhuriwa na maelfu ya wananchi kutoka ndani na nje ya wilaya hiyo.

Kabla ya dua hiyo ilitanguliwa na Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika asubuhi yaliyowakutanisha masheikh mbalimbali waandamizi wakiwemo wa mikoa ya Arusha, Kigoma, Kagera, Dar es Salaam na Pwani.

Katika dua hiyo ujumbe mkubwa uliotawala ni amani ambapo Watanzania wamesisitizwa kuitunza ili kuunga mkono jitahada za Rais Samia ambaye kwa nyakati tofauti amekuwa mstari wa mbele kuhubiri amani.

Mbali na hilo, suala la maadili limesisitizwa kwa kiwango kikubwa kwa kuelezwa kuwa ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha anatunza na kuyalinda maadili kwa manufaa Taifa.

 
Back
Top Bottom