Scaramanga
JF-Expert Member
- Aug 19, 2020
- 490
- 704
Nichukue fursa hii kwanza kukupongeza kwa kuteuliwa kwako kushika nafasi ya Waziri wa Ujenzi. Ni imani yangu kuwa Mhe. Rais kakuamini katika utendaji wako wa kazi na nina imani kuwa utamsaidia sana kwenye eneo la ujenzi.
Nina kilio changu naomba uanze na kuangalia eneo la Kigamboni. Kuna barabara zilikuwa hazina changamoto sana ila wasiamamizi wa barabara Tanroad waliamua kuzichimbua kwa lengo la kurekebisha ila yapata miezi sasa hakuna chochote kilichofanyika na imekuwa ni kero kwa wenye gari , pikipiki na hata watemeba kwa miguu. Hizi mvua zilizonyesha imekuwa haifai kabisa ni mashimo makubwa .
Sina shaka na nia ya kujenga vizuri ila kinachosikitisha ni miezi sasa na kama kulikuwa hakuna fedha bora wangeacha ilivyokuwa mwanzo. Kipande cha kutoka mzunguko wa Darajani kwenda Kisiwani, karibu na ofisi ya mkuu wa wilaya Geza, Kibada kote huko njia wamefumua na kuziacha na zimekuwa ni kero mno.