Ah!!
Ndugu yangu Mathayo Mbatizaji naona unataka kumuonea tu Da' Ummy!!
Sote tunajua wizara walishabadilika na kuanza kutoa ripoti takribani mara 3 kwa wiki!
Nadhani hadi sasa wangekuwa wanafanya kama wenzetu na kutoa updates kila siku!!
Lakini sote pia tunakumbuka, kabla hawajafika mbali na huo utaratibu, Magu akatoa speech, speech ambayo ili-conclude mabadiliko wizara ya afya!!
Baada ya hapo, tukarudi tulikotoka!! Tukarudi tulikotoka kwa sababu alichokusudia Magu kwenye mabadiliko yale ni kupiga marufuku updates za mara kwa mara, na ikibidi zisitolewe kabisa ili ionekane hakuna maambukizi mapya!!
But like I said in one of my posts, this's suicide!!
Ni bure wizara iendelee kutoa updates hata kama namba itakuwa inaongezeka but at least tutaoneka tupo serious!
Kinyume chake, Tanzania itaonekana inafanya cover up, na matokeo yake, hata kama hali sehemu zingine itaonekana imetengemaa bado mataifa makubwa yataendelea kutoa tahadhali kwa wananchi wao kutembelea Tanzania kwa sababu watakuwa hawana taarifa sahihi!
Bora wajue Dar kuna maambukizi 1M lakini Arusha kuna maambukizi 5000, kuliko kutojua lolote kuhusu popote!!