Waziri Ummy: Kigezo kikubwa ambacho tutakitumia kuajiri walimu ni wale wanaojitolea. Alalamikia barua feki

Waziri Ummy: Kigezo kikubwa ambacho tutakitumia kuajiri walimu ni wale wanaojitolea. Alalamikia barua feki

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu amesema yapo malalamiko kuwa baadhi ya Walimu wanaojitolea wanawasilisha barua feki zinazosema wanafanya hivyo wakati hawajitolei.

Ametoa kauli hiyo leo Mei 25, 2021 Bungeni Dodoma wakati akimjibu Mbunge wa Longido Kiruswa aliyehoji ni kwanini Seikali isiajiri Walimu ambao wanajitolea. Amesema hata Wanaojitolea watafanyiwa uchambuzi ili kuona kama ni kweli wanafanya hivyo.

Amesema kigezo kikubwa kitakachotumika ni hicho akiongeza kuwa, suala hilo ni tete ambapo nafasi ni 6,949 ilihali mpaka Mei 23, 2021 walioomba ni 89,958. Ameomba Serikali iaminiwe akisisitiza Haki itatendeka.

========

Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu akibu swali la mbunge Kiruswa lililouliza 'Kwanini wasiajiri walimu ambao wanajitolea?' kwenye ajira za ualimu zilizotangazwa karibuni, amesema kigezo kikubwa ambacho watakitumia katika kuangalia wenye vigezo ni wale ambao wanajitolea.

Waziri Ummy amesema kwa sasa ipo changamoto kwa wengine kuleta bara feki kwamba wanajitolea na suala hilo ni tete kwani nafasi zipo 6,949 lakini walioomba wameshafika 89,958 na kumuomba spika aiamini serikali itatenda haki.

Amesema pia upo mtazamo ndani ya wazira labda waajiri ambao wamemaliza muda mrefu lakini hawajaajiriwa akitolea mfano waliomaliza 2012 kwani muda wao wa kuajiriwa serikalini nao unapungua ambapo wanatakiwa kuajiriwa kabla ya kufikisha umri wa miaka 45.

Mfumo aliouacha JK urudishwe ili tuondokane na haya malumbano.

Unaenda kujitolea halafu hupati hata 400 ya nauli, sasa mahitaji mengine utayatoa wapi?

Ndio maana watu wanaamua kutojitolea ili watafute njia ya kujikimu, na hizi fursa zikitoka na kusikia waliojitolea watapewa kipaumbele lazima watafute uchochoro na wao waonekane kama waliwahi kujitolea
 
Huu ujinga ni Tanzania tu, kwa sheria ipi? Ni lini serikali iliwataka wahitimu wakajitolee na malazi na posho ya kujikimu nani aligharamia? Huu upumbavu utengenezeni tu ipo siku mtafurushwa kwa maandamano na riots.
 
Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu akibu swali la mbunge Kiruswa lililouliza 'Kwanini wasiajiri walimu ambao wanajitolea?' kwenye ajira za ualimu zilizotangazwa karibuni, amesema kigezo kikubwa ambacho watakitumia katika kuangalia wenye vigezo ni wale ambao wanajitolea...
Ninashauri, walioomba na wakakosa ni vema wakajibiwa kwamba wamekosa na wakapewa sababu za kukosa, waliopata vile vile wajibiwe kuwa wamepata na sababu za kupata kuliko ukimya uliopo, unafanya mamilioni ya watafuta kazi kulalamika mitaani.

Pili, mfumo huo uangalie gender pia, kuna uwezekano kuajiriwa gender moja tu. Kwa ujumla mfumo wa ajira uangalie mikoa, wilaya, dini, umri, ufaulu, wenye mikopo, yatima, uwezo wa kifamilia, masomo yenye manufaa kwa sasa, ulemavu, uraia, nk.
 
Ninashauri,waliomba na wakakosa ni vema wakajibiwa kwamba wamekosa na wakapewa sababu za kukosa,waliopata vile vile wajibiwe kuwa wamepata na sababu za kupata,kuliko ukimya uliopo...
Kwenye suala la mrejesho ni vyema watumie huu mfumo wa maombi kujulisha watu wote walioomba kama wamepata nafasi au la pamoja na sababu za kupata au kukosa.
 
Ninashauri,waliomba na wakakosa ni vema wakajibiwa kwamba wamekosa na wakapewa sababu za kukosa,waliopata vile vile wajibiwe kuwa wamepata na sababu za kupata,kuliko ukimya uliopo,unafanya mamilioni ya watafuta kazi kulalamika mitaani. Pili, mfumo huo uangalie gender pia,kuna uwezekano kuajiriwa gender moja tu. Kwa ujumla mfumo wa ajira uangalie mikoa,wilaya,dini, umri ,ufaulu, wenye mikopo, yatima, uwezo wa kifamilia, masomo yenye manufaa kwa sasa,ulemavu,uraia, nk.
Point kabisa
 
Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu amesema yapo malalamiko kuwa baadhi ya Walimu wanaojitolea wanawasilisha barua feki zinazosema wanafanya hivyo wakati hawajitolei

Ametoa kauli hiyo leo Mei 25, 2021 Bungeni Dodoma wakati akimjibu Mbunge wa Longido Kiruswa aliyehoji ni kwanini Seikali isiajiri Walimu ambao wanajitolea. Amesema hata Wanaojitolea watafanyiwa uchambuzi ili kuona kama ni kweli wanafanya hivyo

Amesema kigezo kikubwa kitakachotumika ni hicho akiongeza kuwa, suala hilo ni tete ambapo nafasi ni 6,949 ilihali mpaka Mei 23, 2021 walioomba ni 89,958. Ameomba Serikali iaminiwe akisisitiza Haki itatendeka

========
Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu akibu swali la mbunge Kiruswa lililouliza 'Kwanini wasiajiri walimu ambao wanajitolea?' kwenye ajira za ualimu zilizotangazwa karibuni, amesema kigezo kikubwa ambacho watakitumia katika kuangalia wenye vigezo ni wale ambao wanajitolea.

Waziri Ummy amesema kwa sasa ipo changamoto kwa wengine kuleta bara feki kwamba wanajitolea na suala hilo ni tete kwani nafasi zipo 6,949 lakini walioomba wameshafika 89,958 na kumuomba spika aiamini serikali itatenda haki.

Amesema pia upo mtazamo ndani ya wazira labda waajiri ambao wamemaliza muda mrefu lakini hawajaajiriwa akitolea mfano waliomaliza 2012 kwani muda wao wa kuajiriwa serikalini nao unapungua ambapo wanatakiwa kuajiriwa kabla ya kufikisha umri wa miaka 45.

Alalamikia barua feki? Kwanini kwenye mfumo waliojitolea wasitume recommendations letter ya eneo au shule aliyekuwa anajitolea? Kwanini barua hizo hazikupita kwa Wakurugenzi, madc wa maeneo husika? TSC wapo, TISS wapo, wakaguzi wa shule wapo, maafisa elimu wapo, Ummy mwalimu angalia sasa usiniangushe. Bora ajira zichelewe ila tena haki bin haki.
 
Alalamikia barua feki? Kwanini kwenye mfumo waliojitolea wasitume recommendations letter ya eneo au shule aliyekuwa anajitolea? Kwanini barua hizo hazikupita kwa Wakurugenzi,madc wa maeneo husika ? TSC wapo, TISS wapo, wakaguzi wa shule wapo, maafisaelimu wapo, Ummy mwalimu angalia sasa usiniangushe .bora ajira zichelewa ilabtena haki bin haki.
Wanatafuta namna ya kuwatoa watoto wa maskini hawa wapuuzi.
 
Mfumo aliouacha JK urudishwe ili tuondokane na haya malumbano.

Unaenda kujitolea halafu hupati hata 400 ya nauli, sasa mahitaji mengine utayatoa wapi?

Ndio maana watu wanaamua kutojitolea ili watafute njia ya kujikimu, na hizi fursa zikitoka na kusikia waliojitolea watapewa kipaumbele lazima watafute uchochoro na wao waonekane kama waliwahi kujitolea
Hatari tupu yaan.
 
Back
Top Bottom