Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Ni kuhusu huduma za mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) - Dodoma, Septemba 1, 2022
Kuna ongezeko kubwa la idadi ya wahanga wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza nchini. Hii inaongeza mzigo wa gharama za matibabu kwa Serikali na watu binafsi. Magonjwa haya ni tofauti na mengine kwani mgonjwa hudumu nayo kwa muda mrefu.
Jukumu la kwanza la wizara ya afya ni kuwakinga watu wasiugue. Hivi sasa nchini Tanzania kuna ongezeko kubwa la wagonjwa hasa wenye magonjwa yasiyo ya kuambukiza, watu hawa wanaongeza hatari ya kuufilisi mfuko wa bima ya taifa.
Matumizi na gharama za kushughulikia magonjwa haya zinazidi uwezo wa fedha zinazokusanywa na NHIF. Ni lazima sasa tuwekeze kwenye kijikinga zaidi kuliko kutibu.
Mfano, watu wapunguze matumizi makubwa ya sukari, sigara, chumvi, mafuta pamoja na kunywa pombe kupita kiasi. Aidha, watu wafanye mazoezi. Tusipopabili mbinu NHIF itaelemewa, itashindwa kutoa huduma.
Mwanzoni ilikuwa na lengo la kusaidia watumishi wa umma pekee, lakini mabadiliko ya sheria yaliruhusu watu wengine kujiunga kwa hiari. Watu hawa kwa idadi kubwa wanajiunga wakiwa wagonjwa tayari.
Mfano, Toto afya kadi ina wanachama 186,000. Fikiria visa vya baadhi ya watoto ambao siku hizi wanazaliwa wakiwa hawana njia ya haja kubwa. Gharama ya matibabu ni kama 1,200,000/= huku yeye amelipia 54,000/=. Gharama hizi ni kubwa.
Idadi ndogo ya wanachama ndiyo inafanya NHIF ikose fedha za kutosha ndiyo maana serikali inapanga kuleta sheria ya bima kwa wote ili kuondoa mzigo huu kupitia kuchangiana. Kwa sasa kuna wanufaika milioni 4.8 tofauti na laki 6 ambayo ilianza nao.
Kumekuwepo pia na udanganyifu mkubwa miongoni mwa watoa huduma kwa kutoa huduma zisizo za lazima pamoja na dawa nyingi kwa wagonjwa kisa tu wana bima. Pia, baadhi ya maafisa wa NHIF hushirikiana na watoa huduma kuihujumu NHIF kwa kuandika madeni makubwa kinyume cha hali halisi. Watu hawa hawana nia njema na mfuko huu, wanataka utajiri wa haraka hivyo sheria kali zitachukuliwa kwa watu wenye nia hii ovu.
Mfano mwingine unaoleta mzigo mkubwa kwa NHIF ni watu kubadilisha wanufaika wa mfuko huu. Baadhi ya watu huwatoa watoto ambao mara nyingi huwa hawaumwi na kuingiza mama mkwe mwenye magojwa sugu (Mfano) . Huu ni mzigo mwingine mkubwa.
Pamoja na uwepo wa changamoto zote hizi, Serikali imewatoa hofu wanufaika kwa kutoa uhakika kuwa imejipanga katika kuusimamia mfuko huu ili usife kwa kupitia upya mapendekezo ya mifumo ya tehama, kubadili taratibu za upimaji wa magonjwa (hasa kwa watu wenye magonjwa yanayo fahamika) pamoja na kuongeza idadi ya watumiaji wa mfuko huu.
Akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua ni jinsi gani bima ya afya kwa wote itawafikia watanzania wote, Waziri Ummy amesisitiza kuwa bima hii itakuwa inachangiwa kiasi kidogo tu cha pesa ili kuwafanya hata watanzania wenye hali duni waweze kunufaika. Aidha, wataweka mfumo na utaratibu rafiki wa kuwafikia kwa urahisi.
Ni asilimia 8 tu ya watanzania ndiyo wanatumia NHIF