Waziri Ummy Mwalimu aagiza kata ya Kinaga Kahama kuwekwa kata za kimkakati

Waziri Ummy Mwalimu aagiza kata ya Kinaga Kahama kuwekwa kata za kimkakati

UGANDA

Member
Joined
Jul 24, 2017
Posts
71
Reaction score
75
Waziri Ummy Aagiza Kata ya Kinaga- Kahama kuwekwa katika Orodha ya Kata za Kimkakati itakayojengewa Kituo cha Afya

Wahenga husema usiibe kabla Jua halijazama,pengine ndio kauli inayofaa kusemwa kwa Wananchi wa Kata ya Kinaga iliyopo pembezoni mwa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Katikati ya kukata tamaa kusikoelezeka kwa wananchi wa Kata ya Kinaga wanaofikia idadi ya Elfu kumi na sita (16,000)kwa mujibu wa Taarifa za Manispaa ya Kahama,Uzinduzi wa Nyumba sita za Walimu uliofanywa na Waziri wa Tamisemi Ummy Mwalimu unaleta Ahueni ya kipekee kwao.

“Hongereni sana kwa Juhudi za kujenga kuboresha Miundombinu ya Kusomea watoto wetu mnazofanya ni Matumaini yangu kuwa Nyumba hizi tunazozindua leo kwaajili ya Walimu wetu zitachochea Ufaulu wa watoto wetu kwakuwa sasa Walimu watafundisha pasipo adha ya kuwaza Makazi”Amesema Ummy Mwalimu Waziri wa Tamisemi.

Baadae Waziri Ummy akamuagiza Naibu Katibu Mkuu Tamisemi Dk. Grace Maghembe Kuingiza Kata ya Kinaga kwenye orodha ya Kata za Kimkakati ili iweze kupatiwa fedha za Ujenzi wa Kituo cha Afya kitakachosaidia Akinamama Wajawazito kujifungua salama pasipo vikwazo.

Pamoja na Ahueni ya Kujengewa kituo cha Afya lakini pia Waziri Ummy amemuelekeza Katibu Mkuu Tamisemi,Prof. Rizik Shemdoe kuwaagiza Tarura kuijenga barabara ya Magobeko kwakiwango cha Changarawe ili iweze kupitika wakati wote.

Kwaupande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philmon Sengati amesema Mkoa huo utendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya Kimaendeleo ikiwemo kusogeza karibu Huduma za Afya na kuboresha Miundombinu ya Barabara.

Kata ya Kinaga Katika Manispaa ya Kahama ndio kata iliyopo pembezoni kuliko ikiwa na umbali wa Km 22 kutoka Makao Makuu ya Halmashauro ya Kahama.
IMG-20210829-WA0105.jpg
IMG-20210829-WA0104.jpg
IMG-20210829-WA0103.jpg
 
Kimsingi ndo namuelewa polepole, maana pamoja na kahama kuwa na mgodi mkubwa wenye madini ya dhahabu kwa kiwango kikubwa wanananchi wake Ni masikini, Sasa hapo jiulize nani mzembe?? Cjui waafrika tutaamka lini,

Yaan tumeshindwa kuwaambia hao wachimbaji kwamba, Kama hamtoi walao 10% ya mapato yenu hata kwa robo hakuna kuwekeza??

Anyway tatzo Ni kuwa mkataba unasainiwa ulaya, ukiwa kwenye hotel nzr na luzuku juu, halafu na kiburudisho mrua kabisa baada ya kazi, utawakumbuka kwel wtz??
 
Wewe nawe boya kabisa! Unawezaje kimwamini mtu mnafiki kama polepole?

Alipopewa ulaji na Magufuli,akaukana msimamo wake wa katiba mpya. Polepole ni mganga njaa tu mjinga mjinga.

Migodi ya dhahabu wanalipa kodi vizuri tu serikali kuu. Kodi hiyo inatumika kwa shughuli za maendeleo kwa nchi nzima. Halikadhalika,migodi inalipa pesa nyingi tu kwenye hakimashauri husika. Maendeleo ya Manispaa ya Kahama yamechangiwa mno na uwepo wa migodi ya dhahabu ya Bulyanhulu na Buzwagi.
 
Mkuu mbna unataukana tu, Kwan huwezi kuchangia bila kumtukana mtu?? Ukisema tu hoja zako kinzani hutakuwa umenukuu nilichoongea?? Au ukitukana ndo unapata Amani moyoni??
 
Kila kwenye uhitaji itakuwa ni kata ya kimkakati?

Serikali iache ujinga mahitaji ni makubwa watafute pesa zikafanye Kazi badala ya kutumia maneno ya kijinga.Bora hata useme kata za kipaombele.
 
Kuna chart nilibahatika kuiona ,inaonyesha Tanzania tuna average iq ya 72 ambayo kwA kitaalamu hyo namba ni mtu ambaye ni "almost retarded"..pengine vitu vingine hatuwezi kuendelea kwasababu iq zetu na za viongozi wetu ni ndogo....

Hivi huu upumbavu wa kufanya kila eneo liwe kata,mkoa au wilaya Ili huduma zisogeee ni nani aliuanzisha?
 
Mji wa kahama unamachimbo madogo madogo ndio yaleta mzunguko hapo kahama kuhusu migodi mikubwa inahudumia kata inayozunguka mgodi sio kata zote
 
Back
Top Bottom