Mh Waziri Ummy Mwalimu Yapata mwezi na nusu sasa mfumo wa makato ya mishahara ya watumishi wa manispaa ya Ilala na Temeke haifanyi kazi, kiasi kwamba watumishi walio katika hizo manispaa wanaotaka kuchukua mikopo wamekwama yapata mwezi na nusu sasa, tunaambiwa system ya RASSON imeharibika, hivi hakuna watu wa IT wanaoshughulikia hili swala?au ni hujuma za makusudi, na kwanini iwe ni kwenye manispaa hizi mbili tu?na kwanini itokee kipindi hiki tu?mbona haya mambo hayajawahi kutokea kwa takribani miaka 20 sasa? Tunaomba sana mheshimiwa waziri tusaidie kwa hili, mh Rais amekuamini amekupa dhamana kubwa sana, tuna imani utashughulikia hili swala kwa umakini huenda ni hujuma za makusudi kabisa