Waziri Ummy Mwalimu kupunguza idadi ya idara ndani ya Halmashauri nchini ili kupunguza matumizi na kuongeza ufanisi

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Mh. Waziri Ummy Mwalimu. Pamoja na jitihada zako za kupambana na tamisemi, ni vema sasa ukapunguza idadi ya idara zilizopo ndani ya Halmashauri na kuongeza vitengo zaidi ilu kupunguza matumizi na kuongeza utendaji. Mfano, kuunganisha idara ya elimu msingi na elimu secondary kuwa idàra moja ya Elimu.

Pili maendeleo ya jamii na afya kuwa idàra moja Ila maendeleo ya jamii iwe kitengo. Idara ya mipango na fedha kuwa moja. Idara ya mipango kuwa kitengo. Pia ukumbuke wakuu wa idara hulipwa mishahara mikubwa bila ufanisi wowote.
 
Mbona hata mwendazake alitaka kupunguza matumizi serikalini matokeo yake yakamshinda, hii nchi bana, na wabunge wanalalamika mishahara haiwatoshi. mitano tena kwaooooooooooo
 
Mleta mada upo sahihi kabisa.

Afisa Elimu anatakiwa awe mmoja,kuwe na SLO wa sekondari na msingi,TAALUMA sekondari na msingi.

Halikadhalika wizara ya afya na maendeleo ya jamii awepo mmoja.

Utitiri wa wakuu wa idara kwenye halmashauri ni kuiongezea serikali mzigo usio na tija.
 
Wakuu wa idara ni mzigo ndani ya Halmashauri nchini kuanzia mishahara ,mafuta,magari,ofisi Huku utendaji na ukusanyaji wa mapato tukiambulia zero.
 
Mleta mada upo sahihi kabisa.
Afisa Elimu anatakiwa awe mmoja,kuwe na SLO wa sekondari na msingi,TAALUMA sekondari na msingi.
Halikadhalika wizara ya afya na maendeleo ya jamii awepo mmoja.
Utitiri wa wakuu wa idara kwenye halmashauri ni kuiongezea serikali mzigo usio na tija.
Mfano kuna halmshauri ziko mjini hakuna nyuki Wala misitu unakuta kuna mkuu wa idara au kitendo Cha nyuki na misitu.
 
Hayo matumizi ni kwenye Halmashauri tu! Kwa nini usishauri kurejeshwa kwa Rasimu ya Katiba ya Wananchi ambayo ilifuta vyeo vya hovyo kama vya Wakuu wa Wilaya na Mikoa, ili kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ya kodi za wananchi?

Kabla ya kutaka hizo Idara ziunganishwe tena, ulishawahi kutafuta sababu zilizo sababisha kutenganishwa? Halafu hiyo mishahara mikubwa ya hao wakuu wa Idara ni kiasi gani?

Ni mara ngapi ya mishahara ya Wakuu wa Wilaya, Mikoa, Wabunge na Wakurungenzi wa Mashirika ya umma na Taasisi za Serikali?
 
Mleta mada upo sahihi kabisa.
Afisa Elimu anatakiwa awe mmoja,kuwe na SLO wa sekondari na msingi,TAALUMA sekondari na msingi.
Halikadhalika wizara ya afya na maendeleo ya jamii awepo mmoja.
Utitiri wa wakuu wa idara kwenye halmashauri ni kuiongezea serikali mzigo usio na tija.
Haiwezekani kuunganisha hizi idara elimu sekondari na elimu msingi na haiwesekani kuunganisha maendeleo ya jamii na idara ya afya kwa tunao jua uhalisia tanajua kwa nini haiwezekani
 
Hayo matumizi ni kwenye Halmashauri tu! Kwa nini usishauri kurejeshwa kwa Rasimu ya Katiba ya Wananchi ambayo ilifuta vyeo vya hovyo kama vya Wakuu wa Wilaya na Mikoa, ili kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ya kodi za wananchi?

Kabla ya kutaka hizo Idara ziunganishwe tena, ulishawahi kutafuta sababu zilizo sababisha kutenganishwa? Halafu hiyo mishahara mikubwa ya hao wakuu wa Idara ni kiasi gani?

Ni mara ngapi ya mishahara ya Wakuu wa Wilaya, Mikoa, Wabunge na Wakurungenzi wa Mashirika ya umma na Taasisi za Serikali?
Mke wa JK ndiye chanzo Cha kutenganishwa kwa idara za elimu,zilikuwa sababu za kisasisa. Wakuu wa idara wote wanakipwa over 3.5 milion @
 
Wewe ni muongo mkubwa! Over 3.5 milion!! Yaani Maafisa wa Halmashauri wanalipwa mshahara sawa na DED wao!!
 
Haiwezekani kuunganisha hizi idara elimu sekondari na elimu msingi na haiwesekani kuunganisha maendeleo ya jamii na idara ya afya kwa tunao jua uhalisia tanajua kwa nini haiwezekani
Kwanini hazifai kuunganisha?
 
Kuna changamoto kubwa kwenye kuunganisha idara.

Km lengo kupunguza matumizi tungeanza na idadi ya mawaziri, posho za wabunge na mshahara yao yaani staili zao na halmashauri km vipi idara zifutwe kila kitengo kijitegemee ili kupata uwezo uwajibikaji na ufanisi na kupunguza matumizi unless otherwise mkuu wa idara ni mratibu km lengo ni ufanisi basi mfano fedha na mipango fedha isiwe idara na mipango isiwe kitengo bali vyote viwili viwe vitengo na mkuu wa idara ababe jina la idara.na anaweza toka fedha au mipango.
 
Idara ndani ya Halmashauri ni mchwa unaokula Hadi mabati
 
Back
Top Bottom