DOKEZO Waziri Ummy Mwalimu, tunaomba uingilie kati, Zahanati ya Hosiana Mission Tabora tunanyanyaswa na uongozi wa mkoa

DOKEZO Waziri Ummy Mwalimu, tunaomba uingilie kati, Zahanati ya Hosiana Mission Tabora tunanyanyaswa na uongozi wa mkoa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Jeep wrangler

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2024
Posts
524
Reaction score
1,093
Utangulizi:

Kituo cha Hosiana mission dispensary kinapatikana katika Manispaa ya Tabora.

Kituo hiki cha afya kimekuwa ni kimbilio kwa watu wenye matatizo mbalimbali ndani na nje ya manispaa ya Tabora. Kituo hiki kina madaktari, wauguzi na watumiahi wengine wasiopungua 10.

Baada ya maelezo hayo naomba nieleze jinsi ambavyo kituo cha hosiana mission dispensary kimekuwa kikishambuliwa mpaka kifungwa tarehe 25/5/2024 ambapo mpaka sasa hakijafunguliwa.

Kufungwa kwa kituo chetu kulianza na ujio wa naibu waziri wa afya Dr. Mollel mwanzoni mwa mwezi wa tano, akiongea na wafanyakazi wa hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete na kusema kwamba kumekuwa na uongozi mbovu, na matumi zi mabaya fedha, uchafu huduma zisizo ridhisha katika hospitali ya mkoa nakusema watabadii uongozi na kuwawajibisha kila mwenye kuhusika kuhujumu kitete.

Alipomaliza kuongea hayo aliuliza kuna zahanati inaitwa Hosiana mnaifahamu?

Mmiliki wake ni mwejiriwa hapa mnamjua?

KIsha akamuuliza mganga mfawidhi Dr. mark waziri, wa wakati huo kuwa wanazo taarifa pia kuwa zahanati hiyo inatumia vifaa vya kitete na kusema akimaliza kikao anatembelea zahanati hiyo wakikuta vifaa vya kitete angeifunga dispensary hiyo mwenyewe.

Kulingana na tunachoamini kuwa ni ratiba zake kubana hakufika badala yake aliagiza kwamba ROM na mkuu wa wilaya wafanyie kazi yote aliyo yasema na wao ndio wangeiongoza hospitali mpaka uongozi mpya utakapoletwa na kuwa baada ya wiki angerudi tena ambapo hakurudi.

Ni baada ya tamko hilo kituo cha Hosiana kikaanza kufuatiliwa na kuwindwa windwa kila siku na watu walio rasmi na wasio rasmi wakitumwa kuichunguza dispensary yetu.

Tunashukuru kuwa TAKUKURU na TMDA walitumwa pia, ambapo walichukua vifaa vyote vya dispensary kwa ajili ya uchunguzi kuhusu madai ya naibu waziri wa afya.

Pamoja na kuchukua vifaa kwa uchunguzi wa vifaa tiba pia walihitaji nyaraka zote za mamanunuzi na mauzo ya dawa na vifaa tiba vyetu kwa zaidi ya mie zi 6.

Baada ya TAKUKURU na TMDA kukamilisha uchunguzi wao uliochukua miezi 6 hawakugundua ubadhirifu wala wizi wala kuthibitisha madai ya naibu waziri na badala yake tulikabidhiwa vifaa vyote na nyaraka.

Baada ya uchunguzi huo kukamilika, ziliendelea fitina za hapa na pale kutoka mkoani na hujuma za mara kwa mara zenye lengo la kutafuta sababu tu za kufunga kituo chetu. (mambo mengine mabaya tuyofanyiwa haifai hata kuandika hapa)

Mashambulizi haya yaliendelea kwa mwendo wa wiki tatu na tarehe 23/5/2024 saa 3 kasoro usiku walikuja RMO na DMO kwa kushtukiza na walienda moja kwa moja vyumba vya kupumzishia wagonjwa.

Walipofika ofisini walipitiliza moja kwa kwenye vyumba vya kupumzishia wagonjwa na kuanza kuhoji huduma zinazoendelea.

Walikuwa wakali, hawakuwa tayari kusikiliza na kila maelezo yakitoleawa wanapinga. RMO akatoa agizo la kufunga kituo usiku huohuo wa tarehe 23/5/2023, na saa tano asubuhi ya kesho yake 24/5/2024 wakafunga kituo chetu bila kutupa nafasi ya kusikilizwa.

Tulichukua jukumu la kuwasiliana nao ili kutafuta muafaka lakini DMO akatujibu tunawafungia kwa mda sababu tunahisi mnafanya makosa ambayo tumewaonya awali makosa.

Tulipohoji makosa ya msingi ya kufunga kituo hawana maelezo ya msingi yenye ushahidi zaidi ya maneno ya kuambiwa.

Tuhuma wanazotoa zaidi ni hisia zao na si makosa ya wazi yenye ushahidi bali taarifa na fununu ambozo waliowambia wamewahifadhi na kuwaamini wanatumia taarifa kulazimisha ukiri ili tuhuma zao zithibishwe kwa ukiri wa mashinikizo ya watumishi.

Tuwasiliana na RMO hakutaka kusikiliza na alitoa onyo kuwa asisumbuliwe wala asipigiwe simu.

Hawa ndio viongozi wetu wasiojali huduma na afya za raia wala ajira za wengine. Mnamo tarehe 24/5/2024 RMO alioupigia uongozi akiliuzia maendeleo yetu na kutulisha kuwa uongozi wa mkoa unahitaji kukaa nasi kumaliza.

Tuliitwa mkoani kwa ajili ya mazunguzo na hayakufanyika badala yake RC, RAS, Usalama mkoa mkuu wa wilaya, usalama wilaya na vyombo vyote vya habari walikuja kituoni na kuhoji wafanyakazi kwa kushinikiza na kulazimisha wakiri tulikuwa tunataka kufanya operation na daktari mstaafu alikuwa anamuona mgonjwa ili amfanyie operation kwa kuhoji kwa nini tumewapokea wa walio na rufaa kutoka kitete kwenda bugando wakati usajili hauruhusu kufanya upasuaji mkubwa jambo si kweli hata kidogo.

Katika hii tuhuma..ukweli ni huu hapa; Wakati wagonjwa hao walipopata rufaaa walirudi makwao kwa siku nyingi kutokana na changamoto za kiuchumi maumivu yalipozidi waliletwa na ndugu zao ili huduma za kumuimarisha mgonjwa zifanyike na hakuna mwongozo unaozuia hilo na kumkataa mgonjwa ingekuwa kinyume cha maadili ya utabibu.

Baada ya madaktari kusimamia ukweli bado Mkuu wa mkoa akaagiza viongozi na mmiliki wakamatwe kwa mahojiano kisha wafunguliwe kesi mahakamani lakini taarifa zetu zipelekwe kwenye mabaraza ya maadili MCT.

Tunasikitika kwamba viongozi wetu wamekaa mahabusu siku tatu kwa uonevu huu. Tunatafsiri kuwa kilichotokea kwenye kituo chetu kilipangwa kwa makusudi, hakikutokea kwa nia njema ya kusimamia ubora wa uendeshaji wa huduma za afya unaozingatia taaluma miongozo utu na maadili ya udaktali na tiba katika tasnia ya afya.

Bali kufanya maamuzi magumu yanayotokana na chuki, vita za kugombania madaraka, visasi, wivu mkali wa maendeleo na vinyongo vya watu ambao wamekuwa wakitengeneza taarifa za uongo , uchochezi, ugombanishi, na siasa kwa maslahi binafsi , taarifa zimekuwa zikipelekwa kwenye uongozi mbalimbali ikiwemo ofisi ya RMO zikifika zina aminiwa kwa kuwatumia hao hao tena ndio wachunguzi.

Msingi wa fitina hizi hasa ni kutokana na mmiliki wa Hosiana kuwa mwajiriwa wa Kitete na vita hii inatuumiza sisi madaktari waajiriwa, wauguzi na watumishi wengine ambao kwasasa tumerudi kukaa nyumbani bila sababu za msingi.

Hoja walizozitoa tumezijibia kwenye uchunguzi kwenye baraza la madaktari na wauguzi. Ni mda sasa kituo chetu hakijafunguliwa , tunalipa kodi, pango, tunalipa mishahara ya watumishi, tunalipa NSSF wakati mikataba yetu na wateja mashirika compassion wanatishia kufunga mikataba, jubilee NHIF wanadai turudishe vitendea kazi vyao maana inaelekea miezi mitatu sasa tangu jambo hili kutokea hatujui hatma yetu ni nini Dawa zetu zinaisha muda wake vifaa tiba havitumiki vinachakaa . Mmiliki na familia ya wanazidi kufilisika wafanyakazi wako njia panda hawajui hatma zao.

Tunaomba mamlak husika hasa WAZIRI WA AFYA AINGILIE KATI NA HAKI ITENDEKE. Ndg. Waziri, mmiliki wa Hosiana ni mtu mwadilifu, hana kona wala makando kando yoyote wala hahujumu vifaa vya serikali wala kukwepa chochote au kuvunja taratibu, miiko na taratibu za utabibu.

Tupo tayari kuchunguzwa tena na tena ili haki itendeke na sio kufungiwa bila kusikilizwa.

Tunawasilisha.
 
Waziri wetu Ummy Mwalimu tunaomba utume wataalam wako waje kutusikiliza
 
Kwahiyo wewe unapenda kusikilizwa? Halafu iweje? Hivi kwenye hiyo kada una miaka mingapi? Uliwahi kuona changes gani tokea amekuwa hapo? Jiongeze jombaa
Mshauri aende wapi!

Au akae kimya mkuu?

Naamini Ummy atawasaidia tu.
 
Kuna binti alikuwa hapo nadhani ni CO tu ila alikuwa na dharau mno kwa wagonjwa sasa angekuwa MD sijui ingekuwaje tu, mtu anakuja yupo serious ila hatilii maanani.

Yote kwa yote poleni kwasababu nilipita hapo siku hiyo mchana nikakuta ugeni mkubwa ukiambatana na kucholewa ukutani pafungwe ila kama uchunguzi ukikamilika mambo yatakaa sawa.
 
Kuna binti alikuwa hapo nadhani ni CO tu ila alikuwa na dharau mno kwa wagonjwa sasa angekuwa MD sijui ingekuwaje tu, mtu anakuja yupo serious ila hatilii maanani.

Yote kwa yote poleni kwasababu nilipita hapo siku hiyo mchana nikakuta ugeni mkubwa ukiambatana na kucholewa ukutani pafungwe ila kama uchunguzi ukikamilika mambo yatakaa sawa.
Binti alikosea nini mkuu
 
Back
Top Bottom