Waziri wa ardhi, tulilipia viwanja mwaka 2023 manispaa ya Kigamboni mpaka sasa bado hatujapewa hata kuviona. Je, hii ni sawa?

Waziri wa ardhi, tulilipia viwanja mwaka 2023 manispaa ya Kigamboni mpaka sasa bado hatujapewa hata kuviona. Je, hii ni sawa?

EXPULSION

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2015
Posts
395
Reaction score
292
Kwako WAZIRI wa ARDHI, ndugu Jerry Slaa

Mwaka Jana 2023, miezi ya kukaribia mwisho wa mwaka yalitoka matangazo katika wilaya ya Kigamboni, kuhusu mradi wa viwanja maeneo ya Pemba mnazi.

Masikini mimi nilibahatika kupata fomu ya kiwanja kidogo, kulingana na kipato changu. Kwa bahati nzuri nilifanikiwa kukidhi matakwa ya barua ile, na kumaliza kulipa.

Bahati mbaya mpaka Leo sijui kiwanja kilipo, Wala sijui kinachoendelea. Na sijakabidhiwa hata ya kiwanja mpaka leo.

WAZIRI wa ARDHI sisi watu masikini, tumeona tununue viwanja vilivyopimwa, japo vidogo, je ndio hali hii kwa viwanja hivi.

Tunaomba utusaidie tuonyeshwe maeneo yetu, na tupewe hati zetu

Nawasilisha
1719074477411.jpeg
Pia soma:Kujua hatma ya wananchi kupewa hati ya viwanja vya mradi wa Tundwi Songani vilivyotangazwa na Halmashauri ya Kigamboni na Wizara husika
 
Hii ni kali kuliko!!

Umenunua kiwanja, ambacho hujui kilipo wala hujawahi kukiona?

Mara nyingine Serikali ina kazi kweli kweli.
Kuna watanzania wengine akiona tangazo lolote lile kwenye vyombo vya habari, basi huwa wanaliamini kabisa bila hata ya kulichunguza kwanza, ndiyo maana wapigaji nao wanapita humo humo kwenye matangazo!!
 
Ulilipiaje kiwanja ambacho hujakiona?!
 
Kuna watanzania wengine akiona tangazo lolote lile kwenye vyombo vya habari, basi huwa wanaliamini kabisa bila hata ya kulichunguza kwanza, ndiyo maana wapigaji nao wanapita humo humo kwenye matangazo!!
Kwa akili kama hizi na wapigwe tu kwa kweli.
 
Back
Top Bottom