Waziri wa Elimu Ingilia Kati Wanafunzi Waruhusiwe Kujisajili Vyuoni suala La Ada baadae

Mshangai

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2008
Posts
468
Reaction score
1,086
Usajili wavyuo vingi tarehe za mwisho zinakaribia na kwa vile masharti ni kuwa mpka ada ilipwe zaidi ya nusu wengi watashindwa kujisajili kwa wakati na kupoteza nafasi hii ya kusoma kwa vile hawakupata mikopo.
Taarifa ya kukosa mikopo imewafikia wazazi muda mchache kabla ya vyuo kufunguliwa na kama hali halisi ya maisha ya Watanzania inavyofahamika sio rahisi mtu kumkuta na akiba ya kuweza kutosheleza dharula kama hizo.
Ingekuwa ni jambo la hekima vyuo vikawapokea wanafunzi wote wanaojisajili hata kama hiyo ada aliyonayo haifiki nusu ya ada nzima halafu wazazi wakaendelea kudaiwa na kuwabana wakati wa mitihani kuliko kushindwa kujisajili kabisa.
Nimeona chuo kama Ardhi sharti hilo wamelipa uzito na vijana wengi waliokosa mikopo na wazazi wao hawataweza kulipa kabla ya hiyo tarehe 18/10/2013 waliyoiweka watakosa fursa hiyo.
Huu ni wakati wa kutumia hekima sana hasa kwa hivi vyuo vya Umma,si vema serikali ikaonekana kama inamalengo ya kukomoa raia wake. Maana kama mtu umemnyima haki yake ya mkopo,basi mpe hata nafasi ya kuweza kutafuta atakachoweza kulipa
Bado vyuo vinaweza kuwabana wakati wa mitihani na ada ikalipwa.
 
Hii imezd had chuo changu cha tumain bukoba wanataka bila kulpa lak tano hata kama unamkopo wa 100% huwez sajiriwa
 
mmmmh! ila fikiri vizuri kama mzazi kakosa 7,00,000 toka tarehe 27/sep hivi huko chuo ndio mzazi atapata aweze kulipa nafikiri ifike uangalie kama huna uwezo wa kujilipia basi angalia maisha mengine na ujipange kusoma baadae ila sio kulazimisha kwenda CHUO huku huna uwezo hadi sasa watu wamepita sehem zote kuanzia HESLB-WIZARA YA ELIMU-WAZIRI MKUU-RAIS-UBALOZI WA MAREKANI-CHADEMA-KAMATI YA BUNGE bado majibu ya msaada sio mazuri labda kamati ya Bunge hapo kesho itatoa jibu zuri kwani ndio waliobaki wengine wote hao hawana jibu kwa TATIZO HILI ushauri wangu haya yote maisha jipange utafika jaribu njia nyingine kama huku hakuwezekani sio kulazimisha ilimradi uende chuo huko sio simple simple kama pesa za kuokoteza utakimbia mwenyewe chuoni alaf utajutia gharama ulizotumia na mda wako TAKE CARE
 
Haya bhana naona Elimu sasa imekuwa ghali kuliko kununua vitz ,tutafika kweli?
 
dah, kaka sio ardhi tu UDOM ndio usiseme, nina siku ya 3 leo na sijui hatma yangu maana bila registration hupati room hata kama umeshalipia accomodation, mkopo sina na ada yangu ni 1.2M, natakiwa kulipa 600,000/= for tution fee, 144,000/= for accomodation, 100,000/= medical fee na 5000/= for UDOSO. yaani nimechoka nawaza kurudi maskani nicheki tu mwakani, but nimeshalipa kama 700,000/= lakini wanadai hadi nimalizie
 
Thanx kwa wazo lako, hata mm linanigusa kwan niko UDOM hata sijalipa kitu chochote kwan inanichanganya! ukizingatia mm nategemea Bum.
 
Poleni sana ila nadhani kuna kitu mmejifunza.
1. Bodi ya mikopo si ya kutegemea 100%
2. Akiba haiozi.
3. Vizuri kua na malengo.

Nilipoingia tu form 5 nilijua lazima ntafika chuo sababu nilitamani sana kusoma. Hapo ndipo nilipoanza kujiwekea ka akiba kidogo kidogo kwa ajili ya ada na matumizi nilipomaliza form six wakati nasubiria matokeo nilifanya kazi kwa bidii sana ikiwemo kazi za kilimo ambazo zilikua na hela nzuri tu. Matokeo yalivyotoka nikajikuta njmefaulu kama watu wengine nikaaply tcu na heslb lakini sikubahatika kupata mkopo. Nilitumia kiasi nilichokua navho kulipia ada 1950000 na kingine kwa ajili ya matumizi hapo kila likizo nilikua nikitoka chuo narudi kufanya kazi pia kuna watu nilikuwa nawalipa mashambani wanifanyie kazi wakati mimi nasoma sasa hivi nakaribia kumaliza na sijawahi para shida. So ni ushauri tu saa nyingine serikali si ya kuonea kabisa. Sisi vijana ndio tunatakiwa tujitume tuwe na malengo ili tuweze fanikiwa. Msidharau kilimo na kazi nyingine hasahasa watu wa vijijini maana kilimo kina hela nzuri tu kama ukikifabya kwa moyo.
Ushauri wangu kwa mliokosa mkopo na hamna jinsi msilaumu wala msisumbue serikali kubalini kupoteza mwaka mkajipange upya
 
mimi nimechaguliwa UDOM sijasajiliwa hadi sasa kisa ada na ninategemea bum hadi nimeamua kurudi nyumbani kutafuta kwanza nitakapopata nitarudi chuo kama nitakuwa nimeshachelewa fresh nitaanza mwakani.......!!!!
 
Pole kiongozi hîzi ndo changamoto za kuingia katka mfumo wa IT ,system hii huwa hatambui kiasi kinachopungua nusu,bad enough kila kitu kipo planed hata huku sua imetukumba na inabidi ulipe nusu ya ada pamoja na michango yote ili uwe registered na uwe allocated room.kaka kuhairisha mwaka is not a solution,kama umeweza kulipa laki 7 sidhani kama itashindikana,komaa omba msaada kwa ndugu jamaa ukaze buti.
 

wewe maisha ya Watanzania unayafahamu vizuri?au unasema kwa kwa kuwa umebaatika kumaliza chuu,,,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…