milele amina
JF-Expert Member
- Aug 16, 2024
- 6,045
- 8,080
KAMANDA WA TAKUKURU (M)
MKOA WA KILIMANJARO
S.L.P 1951
Moshi-Kilimanjaro
Imetokea taharuki kuelekea uchaguzi Mkuu October 2025, Moshi Manispaa, baada ya kuonekana mtaani kwa risiti za malipo ya mamilion ya fedha , yasiyojulikana ,zikionyesha malipo kwenda bank ya NMB na risiti zingine za mikono,fedha zinazopingana na kauli ya Rais Dr Samia ,kuwa elimu ni Bure!
Katika , kufuatilia, malalamiko yamekuwa yakiongezeka kuhusu ukosefu wa elimu bure.
Hapa chini, tunaangazia baadhi ya changamoto zinazokabili mradi hewa wa idara ya elimu msingi huko kwa Mwajuma, Moshi Manispaa, Kilimanjaro
Maswali Muhimu
1. Mhasibu wa Mradi: Ni nani anayesimamia fedha za mradi huu?
2. Msimamizi wa Mradi: Je, kuna mtu anayeweza kutajwa kama msimamizi wa mradi huu?
3. Risiti za Malipo: Tunashuhudia matumizi ya risiti nyingi zisizo za kisasa. Baadhi a risiti zinatumika zimepitwa na wakati, wakati wengine wanatumia risiti za mikono.
4. Mitihani hiyo inatungwa na nani na wapi?
5. Mitihani hiyo inasahihishwa na akina na wapi?
6. Mitihani hiyo inatengenezewa wapi?
7. Vyanzo vya fedha hizo zinatokea wapi hadi shule zinatuma huko NMB?
8. Wazazi walishirikishwa lini na kwa njia Gani kutoa michango hiyo?
9. Shule zinazotoa fedha hixo,wanashirikishwa kuandaa bajeti ya mitihani?
10. Shule zinachanga fedha hizo,wanasomewa taarifa ya mapato na matumizi?
11. Mradi huu,wa ukusanyaji fedha kutoka Kila shule,ulianza lini na Hadi Sasa umekusanya billion ngapi? Na fedha ziko wai?
12. Mradi huu unausisha shule zaidi ya 90 Moshi Manispaa, Je ni nani anawasiliana na shule hizo ili fedha ziweze kulipwa?
13. Mkurugenzi wa Moshi manispaa ni mshiriki wa maamuzi ya ukusanyaji wa fedha hizi? Kibali cha kuchangisha fedha hizo kilitoka Kwa nani?
Hii inatoa taswira ya ukosefu wa uwazi na uaminifutunaomba TAKUKURU mlifanyie kazi haraka!
Ufuatiliaji wa Fedha
Ni muhimu kujua ni nani anasimamia mapato na matumizi ya fedha hizi.
Maafisa wa elimu msingi wanapaswa kupewa jukumu la kuchunguzwa jinsi fedha hizi zinavyotumika na nani amewapa mamlaka hayo ya kukusanya mabilioni ya fedha.
Tunahitaji hatua madhubuti na za haraka ili kuhakikisha uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma.
Wito wa Ufuatiliaji
Tunataka ufuatiliaji wa karibu wa fedha za mradi huu. Tunahitaji kuona wahusika wakikamatwa na kupewa adhabu stahiki ili kudhibiti wizi huu mkubwa.
Ras Kilimanjaro, ambaye anadaiwa kupuuza masuala haya, anapaswa kuchunguzwa kwa karibu.
Maswali yanayohitaji majibu ni mengi kuhusu akaunti ya NMB Bank
Kwanza, ni nani signatories wa akaunti hii? Hii ni muhimu ili kuelewa ni nani wanaoendesha akaunti na kufanya maamuzi kuhusu fedha.
Pili, akaunti hii ilianzishwa mwaka gani? Historia ya akaunti inaweza kutoa mwanga kuhusu maendeleo yake.
Aidha, ni kiasi gani cha fedha ambacho kimepitishwa kupitia akaunti hii hadi sasa?
Ni muhimu kujua pia kiasi cha fedha ambacho kipo kwenye akaunti kwa sasa. Hii itasaidia kutathmini jinsi fedha zinavyosimamiwa na matumizi yake.
Kuhusu fedha zinazokusanywa kupitia risiti za mitaani, ni muhimu kujua ni kiasi gani cha fedha kinachokusanywa na kwa nini wanatumia risiti hizo.
Hii inaweza kuonyesha uwazi na uwajibikaji katika ukusanyaji wa fedha.
Swali lingine ni kwanini hatumii control number katika mchakato huu.
Control number inaweza kusaidia katika kufuatilia na kudhibiti fedha zinazoingia na kutoka, hivyo ni muhimu kujua sababu ya kutotumiwa.
Hatimaye, ni nani aliwapa idhini ya kukusanya mamilioni ya fedha?
Hili linaweza kuhusishwa na masuala ya usimamizi na udhibiti wa kifedha, na ni muhimu kujua ni nani waliohusika katika kutoa idhini hiyo.
Maswali haya yanahitaji majibu ili kuleta uwazi na kuelewa vizuri jinsi akaunti ya NMB Bank inavyofanya kazi.
Hitimisho
Kwa ujumla, kuna tatizo kubwa linalohitaji ufumbuzi wa haraka.
Maafisa wote wanahusika na uhujumu huu,wawajibishwe haraka iwezekanavyo,na fedha hizo zirejeshwe shule zilikotoka, na Kuna Kila dalili wamezoea wizi na udanganyifu.
Ni lazima tupate nafasi ya kuanzisha mchakato wa kuchunguza na kufichua ukweli ili kuweza kumshika mchawi.
Tunahitaji umoja katika kupigania haki na uwazi katika sekta ya elimu Moshi Manispaa.
Ombi maalum kwa serikali
Tunaomba fedha za mitihani ya diagnosis, pre-mock, na pre-national kwa shule zote za msingi zisikusanywe tena. Wahusika wanapaswa kupewa onyo kali, na fedha zote walizokusanya zirejeshwe kwa wazazi.
Hali hii imekithiri katika Mkoa wa Kilimanjaro, hasa Moshi Manispaa, na ni lazima hatua madhubuti zichukuliwe dhidi ya wale wanaohusika na zoezi hili.
Mchango wa fedha hizi umekuwa mkubwa na umesababisha madhara makubwa kwa wazazi.
Wazazi wengi wanakabiliwa na mzigo wa madeni yasiyoisha, hali ambayo imepelekea wengine kukimbia ndoa zao au hata kufikia hatua ya kujinyonga.
Hali hii ni ya kusikitisha na inahitaji umakini wa haraka kutoka kwa viongozi wa elimu na serikali.
Tunaamini kuwa sera ya elimu bure inapaswa kutekelezwa kwa vitendo, si kwa maneno matupu.
Tunahitaji kuona mabadiliko halisi ambayo yanaweza kusaidia kuboresha hali ya elimu katika maeneo yetu.
Kila mtoto anapaswa kuwa na haki ya kupata elimu bila vikwazo vya kifedha.
Kwa hivyo, ni muhimu kuhakikisha kuwa fedha zinazokusanywa zinatumika kwa ajili ya maendeleo ya shule na si vinginevyo.
Wazazi wanahitaji kupewa taarifa za wazi kuhusu matumizi ya fedha za shule. Ni muhimu kwa serikali na mamlaka husika kutoa uwazi na uwajibikaji katika masuala haya.
Hili litasaidia kurejesha imani ya jamii katika mfumo wa elimu na kuondoa hofu inayohusiana na michango ya fedha Kila siku kwa ajili ya kujinufaisha watu wachache,na wasio na uadilifu wa roho ya mungu.
Aidha, tunatoa wito kwa viongozi wa elimu, hasa katika TAMISEMI, kwa Kushirikiana na TAKUKURU, kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika.
Wanaweza kufukuzwa kazi au kushushwa vyeo na kuhamishiwa mikoa mingine ili kudhibiti ufisadi na uonevu wa wazazi. Hii itakuwa funzo kwa wengine wanaofanya vitendo kama hivyo.
Hatimaye, tunataka kuwa na mazingira bora ya kujifunzia kwa watoto wetu. Tunaamini kuwa elimu ni msingi wa maendeleo, na tunapaswa kuwekeza katika siku zijazo za watoto wetu.
Tuchukue hatua sasa ili kuhakikisha kila mtoto anapata haki yake ya elimu bila vikwazo vya kifedha.

Attachments
-
IMG-20250208-WA0006.jpg42.4 KB · Views: 3 -
IMG-20250208-WA0011.jpg50.1 KB · Views: 3 -
IMG-20250208-WA0009.jpg38.3 KB · Views: 2 -
IMG-20250208-WA0010.jpg32.1 KB · Views: 2 -
IMG-20250208-WA0007.jpg43.2 KB · Views: 4 -
IMG-20250208-WA0008.jpg41.2 KB · Views: 3 -
IMG-20250208-WA0007.jpg43.2 KB · Views: 3 -
IMG-20250208-WA0011.jpg50.1 KB · Views: 4 -
IMG-20250208-WA0012.jpg64.4 KB · Views: 1 -
IMG-20250208-WA0017.jpg41.2 KB · Views: 3 -
IMG-20250210-WA0060.jpg167.9 KB · Views: 2 -
IMG-20250210-WA0061.jpg66.7 KB · Views: 2 -
IMG-20250210-WA0062.jpg69.2 KB · Views: 4 -
IMG-20250210-WA0063.jpg59.5 KB · Views: 3 -
IMG-20250210-WA0064.jpg54.4 KB · Views: 3 -
CamScanner 02-10-2025 11.46.pdf380.3 KB · Views: 2