Waziri wa Elimu: Udanganyifu wa Mitihani ni sawa na uhujumu uchumi, Watumishi watakaobainika watafukuzwa kazi

Waziri wa Elimu: Udanganyifu wa Mitihani ni sawa na uhujumu uchumi, Watumishi watakaobainika watafukuzwa kazi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Prof. Adolf Mkenda akiwa katika mkutano na waandishi wa habari Dodoma, leo Februari 8, 2023, amesema:

FobmB2UXgAIk5Yl.jpg
“Gharama za kuendesha mitihani ya kitaifa ni kubwa, kufanya udanganyifu ni sawa na uhujumu uchumi hivyo watumishi wa umma watakaobainika kushiriki katika udanganyifu wa mitihani hiyo watachukuliwa hatua kali ikiwemo kufukuzwa kazi na kushtakiwa.

“Jumla ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2022 ni 560,335. Kati yao 337 ambao ni sawa na asilimia 0.06 wamefutiwa matokeo kutokana na udanganyifu. Watahiniwa wengine 20 matokeo yao yamezuiliwa na uchunguzi unaendelea.

“Udanganyifu wa mitihani uliofanyika ni asilimia 0.06 ambao unaonekana ni mdogo, lakini athari yake kwa taifa ni kubwa sana. Jitihada zinafanyika kuumaliza kabisa.”

FobmYTUWAAALJsa.jpg
 
Back
Top Bottom