MFUMUKO MDOGO WA BEI TANZANIA (LOW INFLATION RATE IN TANZANIA 2023)
Tanzania ni kati ya nchi chache Barani Africa zenye mfumuko mdogo wa bei ukilinganisha na nchi nyingine nyingi zenye mfumuko mkubwa wa bei kuanzia 5.0% mpaka 87.6%. mfano (Rwanda 30.3% & Zimbabwe 87.6%)
Katika ripoti iliyotolewa na Bank kuu ya Tanzania(BOT) February 2023 inaonyesha Mfumuko wa bei umeshuka kutoka asilimia 4.9% mwezi January 2023, na kufikia asilimia 4.8% mwezi February2023.
Bank of Tanzania
Pia inaangaziwa kiwango cha 4.8% kitaendelea kushuka katika siku za mbeleni(Forward looking).
Hii ni kutokana na juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais.Dr Samia Suluhu Hassan pamoja na Wizara ya Fedha na Mipango Chini ya Waziri Dr. Mwigulu Nchemba.
SABABU ZA MFUMUKO MDOGO WA BEI TANZANIA
Sera Bora za Fedha; ambazo zinatungwa na kutekelezwa na Bank kuu ya Tanzania(BOT). Benki kuu (BOT) imekuwa ikitekeleza sera mathubuti kuangazia mfumuko mdogo wa bei na kukuza uchumi. Sera hizi ni pamoja na msawazo wa fedha katika mabenki, kudhibiti viwango vya riba. Kufadhili katika shughuli zinazokuza uchumi au shughuli za maendeleo ili kuongeza uzalishaji.
Uwekezaji katika sekta ya kilimo; ili kuongeza uzalishaji. Kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania, unachangia zaidi ya asilimia 30% ya pato la taifa(GDP) na kuajiri zaidi ya asilimia 65% ya nguvu kazi.
Pia ongezeko la wadau na mipango mathubuti inapekelekea kuongezeka kwa uzalishaji katika sekta ya kilimo.
Pia bajeti ya kilimo imeongezwa ili kuleta matokeo chanya katika seketa hii.
Utulivu wa Kisiasa; tunaweza kusema hali ya Utulivu katika siasa umefanya kusiwepo na mfumuko wa bei kwa sababu utulivu wa kisiasa usingekuwepo kwa lugha nyingine ni uwepo wa Vita au Maandamano, Machafuko ambayo yangepelekea kupanda kwa gharama zamaisha na mfumuko wa bei kutokea.
Sekta ya Utalii; pia ni moja ya sekta inayochangia kupungua kwa mfumuko wa bei utalii unaongeza pato la taifa kwa kuongeza stock ya Fedha za kigeni zinazotumika kuweka utulivu wa bei katika nchi. Mchango wa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan katika Documentary ya Royal Tour umepelekea watalii kuongezeka maradufu zaidi.
Sera nzuri za Serikali; zinazolenga kukuza viwanda vya ndani na kupunguza utegemezi wa nchi zingine katika kuagiza bidhaa kutoka nje. Hii imesaidia kuleta utulivu wa kiwango cha bei. Na pia kupunguza utegemezi wa hali ya juu wa bidhaa kutoka nje.
Uwekwaji wa ruzuku; Mchango wa serikali mfano uwekwaji wa ruzuku wa Tsh bill 100 ilikuleta utulivu au unafuu wa bei ya nishati umechangia kwa kiasi kikubwa na kupunguza mfumuko wa bei. Kwa namna nyingine pia tunaona ruzuku ya mbolea imesaidia kuongeza uzalishaji. Haya yote ni utekelezaji wa serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan.
Bank ya Dunia(WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF); Tanzania imekuwa ikishirikiana na haya mashirika ya kimataifa kutekeleza sera za kiuchumi na Kijamii ili kuleta maendeleo katika nyanja muhimu na hii inapelekea kuwa na sera nzuri ili kukabili mfumuko wa bei.
FAIDA ZA MFUMUKO MDOGO WA BEI TANZANIA
Kukua kwa uwekezaji; mfumuko mdogo wa bei unavutia wawekezaji kutoka pande zote za dunia kwani unapunguza hatari ya kushuka kwa thamani ya sarafu na kuhakikisha mapato yanaongezeka kwenye uwekezaji. Pia uwekezaji ukiongezeka unaongeza ajira, kwa namna nyingine uwekezaji unapunguza tatizo la ajira.
Utulivu wa bei:
Mfumuko mdogo wa bei unapelekea kuwepo kwa utulivu wa bei za bidhaa ambazo hazimuumizi mnunuaji na muuzaji. Hii inawanufaisha wananchi kwa kurahisisha maisha.
Kuongezeka kwa uwezo wa kununua:
mfumuko wa bei unaongeza uwezo wa kunua kwa sababu bidhaa zinakuwa sio ghari na zinaruhusu kununua bidhaa kwa kiwango cha pesa kisicho kikubwa ukilinganisha na hapo mwanzo.
Hii inasaidia kuboresha hali ya maisha na kupunguza umaskini.
Unafuu wa Riba:
Ambavyo vinaweza kuwanufaisha wafanyabiashara na wafanyakazi kwa kupunguza gharama ya kukopa pesa. Hii inaweza kuchochea ukuaji wa uchumi na uwekezaji.
Kwa namna moja au nyingine mfumuko mdogo wa bei unasaidia kukuza uchumi kwa kuongeza imani katika uwekezaji pia kuvutia uwekezaji, kuongeza ajira, kuongeza mapato ya nchi, Kuongeza kiasi cha akiba, kuboresha utendaji wa kazi.
MAMBO YANAONEKANA