Pre GE2025 Waziri wa Katiba na Sheria (Ndumbaro): Tanzania inaendelea kwa sababu kuna Haki, Usawa na Amani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Wananchi tuna amani, muda wote ni mwendo wa kububujikwa machozi ya furaha kwa nzuri anayofanya kipenzi chetu Mama Dokta (zitamke mara 9 sikumbuki namba yote) Kipenzi cha Wote Jemedari Amiri Jeshi Mkuu mwenye anaupiga mwingi Samia Suluhu Hassani, au nasema uongo ndugu zangu?

======

Your browser is not able to display this video.


Waziri Damas amesema Tanzania inaendelea kimaendeleo kwa sababu kuna haki, usawa na amani.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro ameyasema hayo wakati akizindua rasmi kampeni ya huduma za Msaada wa kisheria Mama Samia Legal Aids Campaign Mkoani Morogoro, ambayo inatekelezwa katika Wilaya zote za mkoa huo kwa kipindi cha siku 10, kuanzia leo Disemba 13 hadi 22, 2024.
 
Waziri Yupo sahihi sana 🐒
 
Endeleeni tu kuwaona Watanzania mazezeta siku wakichoka mtalia na kusaga meno,mtajuta.
 
Kweli ukiwa ccm lazima ujizime data
 
Kumbe huyu Ndumbaro ni mionhoni mwa wale ambao uchafu wa tumboni umefunika uwezo wa akili kiasi hiki!! Na huyu, kumbe ni hovyo kabisa.

Watu wanalia na kuhuzunika kwa vile ndugu zao wanatekwa, wanauawa hovyo na vyombo vya dola, yeye anaiita hiyo ni haki!! Huu ni ushetani wa hali ya juu. Tunaomba sana majitu haya yanayoshabikia mateso na mauaji ya wananchi yanayofanywa na watawala, laana kubwa ikawe juu ya vichwa vyao.

Mungu wa huruma uwarehemu na kuwapumzisha ndugu zetu wote waliouawa na watawala, na kisasi juu ya wauaji na wapambe wao, ni juu yako.
 
Wamevaa mawani za mbao hawaoni aibu tena
Hili nalo naona ni yale yale, yaliyo mzigo kwa Watanzania. Kwa unafiki huu wa kusifia uovu, anaamini ataonekana kuwa yeye ni bora kuliko mtangulizi wake aliyepelekwa kusimamia ngoma kwa sababu alishindwa kusifia maovu yanayofanywa.
 
Anazungumzia maendeleo binafsi , atakuwa amekula per diem nyingi akisafiri na Taifa Stars😏
Ninavyofahamu duniani hamna haki,pengine tukibahatika kufika mbinguni tu.Hata wapo wanaoamini dunia hii ni ubaya ubwelamwanzo mwisho.
 
Anawakejeli Familia za Watanzania waliotekwa na kuuwawa na wengine wanaonyimwa Haki zao.
 
Anawakejeli Familia za Watanzania waliotekwa na kuuwawa na wengine wanaonyimwa Haki zao.
Watanzania kwakuwa tunaweza yumbishwa kama mbayuwayu,kutoka wizara waipendayo wabongo sasa ni muda wa kuchafua mbongo zao kwani lazima waelewe kama kule maigizoni michezoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…