Waziri wa Maji; Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji jimbo la Sengerema kiti anachokalia sio size yake, akae pembeni

Waziri wa Maji; Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji jimbo la Sengerema kiti anachokalia sio size yake, akae pembeni

cleokippo

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2014
Posts
2,118
Reaction score
1,797
Asalam

Wapo watendaji wa serikali wanafanya kazi kwa mazoea kwa kuamini hakuna mbadala yao. Wapo pia wafanyakazi ambao hawafanyi kazi ipasavyo kwa kuamini kuwa wenye mamlaka ni washkaji zao na hivyo hawana uthubutu wa kuwawajibisha.

Wapo watu wakikaa kwenye system hubweteka na wakiondolewa tu wanalia na kusaga meno kwa kuamini kwamba wameonewa bila kujua kwamba madhaifu yao ndio sababu iliyopelekea kuondolewa kwao.

Kumekuwa na malalamiko ya mara kwa mara toka kwa wateja wapya wanao hitaji kuunganishiwa huduma ya maji kwenye site zao, nyumba zao na miradi mbalimbali ya maendeleao dhidi ya Mamlaka ya Maji ya Sengerema (SEUWASA)

Unakuta mteja analipia gharama zote za kuunganishiwa maji cha kuskitisha mamlaka haimpelekei maji kwa madai kwamba wamesitisha huduma ya kuwaunganishia wateja wapya kutokana na ukosefu wa vifaa kumbe wanatengeneza mazingira ya RUSHWA.

SWALI; kama mamlaka haina vifaa unapokea pesa za nini toka kwa wateja?

Hapo mkurugenzi anapaswa kukubali kabisa kuwa kiti alichokalia si size yake hivyo anawajibu wa kuwapisha wenye uwezo wa kukalia kiti hicho wakae.

Haiwezekani yeye yupo, T.M yupo na afsa manunuzi pia yupo halafu mamlaka ikose materials.

Mara kwa mara tumeona Mh mbunge wa jimbo la sengerema Khamis Tabasam pamoja na madiwani wake wakiwapigia sana kelele watendaji wa mamlaka hiyo ya maji bila mafanikio.

Kwahiyo " kwa niaba ya wateja wote wapya wa kuunganishiwa maji jimbo la Sengerema tunaomba kilio hiki kikufikie popote ulipo MH JUMA AWESO sababu hii ndio sehemu pekee na sahihi ya kusemea kwakuwa wananchi wa chini hatuna huwezo wa kukufikia na kuwasilisha kero zetu kwako.

NOTE: Mkurugenzi wa mamlaka ya maji sengerema anapaswa kuwajibishwa kwani wananchi tumechoshwa na utendaji wake mbovu.
 
Back
Top Bottom