Waziri wa Mambo ya Ndani aagiza Polisi Kanda Maalum ya Dar kumsaka na kumhoji Askofu Mwingira

Waziri wa Mambo ya Ndani aagiza Polisi Kanda Maalum ya Dar kumsaka na kumhoji Askofu Mwingira

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200
"...ni ajabu kama yote hayo alitendewa na bado hakuwasilisha malalamiko kwenye vyombo vya dola inaleta ukakasi."

"...hivi kweli utendewe yote hayo muda wote huo ndiyo usubiri hasi Krismasi useme?!" Amehoji Simbachawene.

"....kwasababu yupo hapa Dar es Salaam na ametoa tuhuma nzito namna ile namuagiza sasa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amwite na amuhoji kuhusu tuhuma hizo." Amesema Simbachawene Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Chanzo Millard Ayo.

=====

Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene ameelekeza Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar kumtafuta Askofu Josephat Mwingira na kupata maelezo zaidi, kufuatia tuhuma mbalimbali alizotoa ikiwemo kutishiwa maisha

Amesema, "Ni tuhuma nzito, zinapotolewa na Kiongozi wa Kijamii/Kidini na ambaye ni maarufu na anajulikana tunapata shida kidogo. Kama matukio haya yote ndivyo yalikuwa yanatokea kwanini hatoi taarifa Polisi ili hatua ziweze kuchukuliwa kuwatafuta wahusika"

Ameongeza, "Tamko la Askofu Mwingira mimi nimelisikia kwenye Mitandao. Nimepata 'clip' lakini sijasikia vizuri maana kama haina sauti. Bado tunaendelea kulifuatilia"

Simbachawene Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, unda tume huru ya kuchunguza kifo cha JPM .
.Usisubiri hadi 2025 wananchi wanahoji na Hakuna majibu na majawabu sahihi kuhusu kifo cha JPM.
Mwenyekiti wa tume hiyo awe Dr Bashiru Ally Kakurwa na mke wa marehemu JPM awe mjumbe wa hiyo tume.
 
"...ni ajabu kama yote hayo alitendewa na bado hakuwasilisha malalamiko kwenye vyombo vya dola inaleta ukakasi."

"...hivi kweli utendewe yote hayo muda wote huo ndiyo usubiri hasi Krismasi useme?!" Amehoji Simbachawene.

"....kwasababu yupo hapa Dar es Salaam na ametoa tuhuma nzito namna ile namuagiza sasa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amwite na amuhoji kuhusu tuhuma hizo." Amesema Simbachawene Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Chanzo Millard Ayo.
Wewe Simbachawene mwenyewe ulitulia kama maji ya mtungi usicheze na Hayati JPM....
Kila kona watu walifyata....itakuwa Mwingira....
Nchi ngumu sana hii...
 
Wewe Simbachawene mwenyewe ulitulia kama maji ya mtungi usicheze na Hayati JPM....
Kila kona watu walifyata....itakuwa Mwingira....
Nchi ngumu sana hii...
Wewe si ulisema Serikali ya sasa haiwezi kuhangaika na Mwingira sasa kiko wapi?!
 
Back
Top Bottom