Waziri wa Mambo ya Ndani aagiza Polisi Kanda Maalum ya Dar kumsaka na kumhoji Askofu Mwingira

Acha kushauri ujinga wewe. Yaani tupoteze fedha za walipa Kodi kuchunguza nn?
 

Na wahusika walazimishwe wamfufue, eeeh!!

Aje aendeleze zile siasa za kikanda, mauaji, kuteka watu, na kuminya haki za watumishi wa umma.

Mfate chato ukalinde kaburi...
 
Wana haki ya kumuhoji, maana tuhuma zimetolewa kwa Serikali....wasiishie tu kumuhoji bali waanzishe uchunguzi dhidi yake juu ya yote anayosema ametendewa ukweli wale ujulikane..
Yaani watuhumiwa wajichunguze? tetetetetete
 
Ni kweli kabisa dini na serikali vinajuana na vinalindana sana ndio mana taasisi za kidini hazitozwi kodi..hizo ni kama fadhila..pia wao watu wa dini kazi kubwa ni kushape moyo ya wananchi ili waendelee kua watii wa serikali..ukiona nchi serikali na dini vinakaa meza moja lengo lao hua ni moja tu kulinda maslahi yao.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ile kauli ya Ikulu inaongozwa na shetani na kiongozi mkuu wa ikulu ni mtoto wa shetani kwakweli sio kauli ya kiungwana hata kidogo. Awajibike kwa kauli hiyo aeleze alimaanisha nini.
 
Naona baada ya Sinema ya Kutuhamisha ya akina Polepole, Nnauye na Mzee Bulembo 'Kubuma' sasa Waziri, Serikali na Mfumo ( System ) wameamua waje na hili wakiamini na wakijidanganya kuwa Watanzania wote ni Wapumbavu sana.
 
Simbachawene anapaswa kufahamu kuwa viongozi wa dini na hasa ya kikristo hutoa majumuisho ya yaliyotokea kipindi cha nyuma na kutoa mapendekezo yao ya mwelekeo ambao wanadhani ni sahihi kwa Taifa ili lisiangamie, na kwa kuwa hii ni Krismas ya kwanza tangu serikali ya awamu ya tano kufa hivyo huu ndiyo muda sahihi wa kutema nyongo.
 
Ile kauli ya Ikulu inaongozwa na shetani na kiongozi mkuu wa ikulu ni mtoto wa shetani kwakweli sio kauli ya kiungwana hata kidogo. Awajibike kwa kauli hiyo aeleze alimaanisha nini.
Serikali ya kifedhuli na kibabe kama hii iliyopo madarakani haipaswi kuambiwa kiungwana bali kukaripiwa!
 
Huyu mjinga alikubali wito wa Jeshi la Polisi imekuaje aamukie airport badala ya kituo cha polisi, watu bado hamjifunzi kusoma alama za nyakati…

Kitendo cha kusema Ikulu ilikuwa na shetani, moja kwa moja amemgusa Mama yetu Samiah Suluhu Hassan maana ndio alikuwa Makamu na Msaidizi wa Hayati shutuma zote mnazomtupia Hayati JPM moja kwa moja zinamgusa Mama pia..

Lazma akayatolee maelezo kauli alizotoa basi..
 
Mpaka chozi. Nabii Mwingira hakupaswa kutoa kauli yenye viashiria kama vile alihusika na kumuua Dkt Magufuli. Yaani taasisi ya urais bado inaomboleza tena kwa machungu kiasi hicho yeye anakuja na mambo ambayo hayawapeleki watu mbinguni
 
Tuleteeni katiba mpya tuepukane na tawala za kibabe, kwa nini kuanza kuwasakama viongozi wa dini..........hivi huko fisiemu mnajiona wasafi hadi kufikia level ya kuwa victimize viongozi wa kidini kisa wameelekeza tuhuma kwenye utendaji wa serikali? kwa hiyo serikali au viongozi wake hawatakiwi kutuhumiwa kwa namna yoyote ile, kwamba wao ni malaika...........
 
Simbachawene aache mihemko ya kijinga, hamna kosa alilofanya Mwingira, Mwingira alichofanya ni kuanika ushetani wa awamu ya tano ambao kila mpenda haki lazima aukemee kwa nguvu zote! Mbona Diallo alisema yule katili alikuwa mgonjwa wa akili na hajaitwa popote kuhojiwa ili adhibitishe kauli yake? Kwa utawala huu Mwingira hawezi kuhojiwa, anatafuta fedheha tu huyo waziri, amuulize mwenzake Gwajima alikurupuka na amri kama hizo kuhusu Bishop Gwajima, akapuuzwa na akaishia kupata aibu!! Huu utawala ongea chochote kile ili mradi huvunji sheria
 
Mpaka chozi. Nabii Mwingira hakupaswa kutoa kauli yenye viashiria kama vile alihusika na kumuua Dkt Magufuli. Yaani taasisi ya urais bado inaomboleza tena kwa machungu kiasi hicho yeye anakuja na mambo ambayo hayawapeleki watu mbinguni
Hakuna mwenye akili anayeombeleza kifo cha Shetani, labda nyie mashetani wenzake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…