Waziri wa Michezo Mchengerwa acha kukurupuka, jifunze zaidi historia za Simba SC na Yanga SC

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Nilishaanza taratibu kukudharau ila kwa ulichokiongea leo katika hafla ya kuwopongeza Tembo Warriors ndiyo nimeamua kukudharau zaidi na rasmi.

Waziri wa Michezo Mchengerwa ni nani kakudanganya kuwa ipo siku au inawezekana vilabu vya Simba SC na Yanga SC kuungana na kusapotiana hasa pale zinapocheza Michuano ya Kimataifa?

Sasa GENTAMYCINE nakuambia kuwa acha kupoteza muda, mimi kama mwana Simba SC kamwe siwezi kuipenda na kuwapenda Yanga SC na wana Yanga.

Unaacha kuiunganisha Taifa Stars ambayo kutwa inakushinda pamoja na juhudi zako za kinafiki/unafiki unataka kugusa vilabu ambavyo huviwezi na hata huvijui vyema kihistoria?

Wewe ni hasara kubwa kiuwaziri.
 
Wale wajinga sitaisahau siku waliyompiga shabiki wa Simba SC pele Taifa wakamchania jezi yake vipande vipande kama kibaka
 
Team zikishakuwa hasimu basi hakunaga maswala ya kutakiana kheri, Ahly&Zamalek , Raja&Wydad zilizoko kwenye mataifa yaliyoendelea zina uhasama ambao Simba Sc na Yanga hazifati hata robo na zimeshindwa kuungana itakuja kuwa hapa Tz?

Haitakuja kutokea kwasababu anguko la team jirani ndiyo furaha isiyo na kifani kwa jirani mwingine, yani mimi niombee Yanga iingie makundi?[emoji23]
 
Uzalendo ulishauliwa na Gongowazi mwaka 1993 kwenye fainali ya CAF Simba SC dhidi ya Stella Abijan na ukaja kuzikwa rasmi na hao hao tena kwa kuwapokea wageni Airport

Leo hii ndo mnaona madhara ya hii dhambi siyo..! Uzalendo utabaki kwenye National Team.
 
Uzalendo kwenye Nt ila huku vilabuni hakuna uzalendo tena
Atafute namna ya kuwafuta machozi uto wakitolewa sudan
 
goli la pili la boli zozo linaingia nyavuni jamaa wanaimba uzalendo umetushinda, kila mara wanashinda airport kupokea wapinzani wa simba kina mwakalebela wanshinda nao hotelini na kuwaambia wasiingie vyumbani kumepuliziwa sumu HALAFU LEO ETI ANATOKEA MTU ANATOA AMRI KUSHIRIKIANA NAO, HATUTAKI SASA
 
Hii haitakuja kukaa sawa kwasababu sumu ilishapandwa kitambo na mpaka sasa ni mwendelezo tu

Si mmeona hata ile kesi ya Barbara Gonzalez kuwa wapinzani wanasaidiwa na watani wetu, kipindi kile Engineer Hersi alipokuwa anawasiliana kwa Video Call na wachezaji wa Barkane, Kisinda na Fiston Abdulrazak huku akiwaambia njooni tutawapokea.

Ilhali akijua kabisa kuwa ni muda mchache Simba SC watacheza na RS Barkane na yeye ni M/kiti wa kamati ya usajili ya Yanga wakati ule.

Na sijui kwanini ile kesi imefunikwa mpaka sasa haieleweki hatima yake..!
 
Wale wajinga sitaisahau siku waliyompiga shabiki wa Simba SC pele Taifa wakamchania jezi yake vipande vipande kama kibaka
Na arusha walimpiga shabiki wa coastal union aliyevaa jezi ya simba mpaka akapoteza uhai hakuna uongozi wala mchezaji aliyeomba msamaha yaani mi siwezi kushabikia yanga hapa naulizia utaratibu wa kwenda Sudan.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…