Natamani hizi shule zinazojengwa kwa mbwembwe nikute mtoto wa Ummy ama mjuu wake anasoma hapo pamoja na watawala wengine wapeleke watoto wao kwenye shule za Umma.
Natamani hizi shule zinazojengwa kwa mbwembwe nikute mtoto wa Ummy ama mjuu wake anasoma hapo pamoja na watawala wengine wapeleke watoto wao kwenye shule za Umma.
Kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake. Usilazimishe na watoto wao wakasomee hizo shule kwani hakuna aliyefanya hivyo na hakuna atayefanya hivyo na hata kama ungekuwa ni wewe usingefanya hivyo. Ww mwenyewe ukiwa na hela unajichagulia chakula kizuri cha kula na hakuna anayekupangia.
Hata hivyo, tunapongeza ujenzi wa madarasa hayo kwani ni msaada mkubwa kwa wengi wenye kipato kidogo. Wengi wetu hapa tumepitia huko, na kama sio hizo shule, huenda tusingeendelea na elimu baada ya primary education