Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) Juni 15, 2024 amefunga rasmi mafunzo ya mwaka mmoja ya Ukamanda na Unadhimu katika Mahafali ya 38 ya Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Tanzania zilizofanyika katika Viwanja vya chuo hicho, Duluti Arusha.
Mahafali hayo ambayo Waziri wa Ulinzi na JKT alikuwa mgeni rasmi yalihusisha Maafisa wahitimu 45 toka Jeshi la Wananchi la Tanzania na Maafisa wahitimu 24 toka nchi marafiki.
Katika Mahafali hayo wahitimu hao pia wa kozi ya Ukamanda na Unadhimu pia walitunukiwa Shahada za Uzamili na stashahada ya Masuala ya Ulinzi na Usalama, mafunzo ambayo yaliendeshwa sambamba na kozi ya ukamanda na unadhimu.
Waziri Tax ametoa salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye chini ya uongozi wake Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepiga hatua kubwa katika demokrasia, utulivu wa kisiasa, amani, usalama, maendeleo ya kijamii na kiuchumi, na uhusiano wa kikanda na kimataifa. akamshukuru sana Rais na Amiri Jeshi Mkuu kwa kumteua kuwa Waziri wa Kwanza Mwanamke wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika Hotuba yake, Waziri wa Ulinzi na JKT amewakumbusha wahitimu kuwa kama viongozi wajao watakabidhiwa majukumu ya kufanya maamuzi muhimu ya ulinzi na usalama wa mataifa yao akawaambia ana uhakika kwamba Elimu na ujuzi walioupata umewatayarisha, na utatumika kama msingi wa utekelezaji wa majukumu yao na kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Mahafali ya 38 ya Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Duluti yalihudhuriwa pia na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Wakuu wa Kamandi za Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Wakuu wa Vyuo ya Ukamaanda na Unadhimu vya Afrika Mashariki, Wakuu wa Vyuo ya Kijeshi ya Jeshi la Wananchi la Tanzania, Waambata Jeshi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania, Maafisa wakuu Majenerali toka Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Makamanda vikosi vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Attachments
-
IMG-20240615-WA0119.jpg223.6 KB · Views: 8 -
IMG-20240615-WA0118.jpg273.5 KB · Views: 5 -
IMG-20240615-WA0122.jpg228.8 KB · Views: 5 -
IMG-20240615-WA0123.jpg222.6 KB · Views: 4 -
IMG-20240615-WA0117.jpg272.2 KB · Views: 6 -
IMG-20240615-WA0112.jpg334.5 KB · Views: 4 -
IMG-20240615-WA0121.jpg511.1 KB · Views: 4 -
IMG-20240615-WA0120.jpg548.2 KB · Views: 5 -
IMG-20240615-WA0114.jpg348.6 KB · Views: 5 -
IMG-20240615-WA0124.jpg500.5 KB · Views: 6 -
IMG-20240615-WA0116.jpg618.9 KB · Views: 5 -
IMG-20240615-WA0115.jpg521.8 KB · Views: 7 -
IMG-20240615-WA0113.jpg391.4 KB · Views: 7 -
IMG-20240615-WA0111.jpg546.9 KB · Views: 6