Waziri wa Ulinzi na JKT aongoza waombolezaji kumuaga Brigedia Jenerali Chakila

Waziri wa Ulinzi na JKT aongoza waombolezaji kumuaga Brigedia Jenerali Chakila

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
WAZIRI WA ULINZI NA JKT AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUMUAGA BRIGEDIA JENERALI CHAKILA

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb), tarehe 26 Juni 2024 ameungana na kuongoza Waombolezaji Katika Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Msalato, jijini Dodoma, kuaga mwili wa marehemu Brigedia Jenerali Andrew Chakila aliyefariki Dunia tarehe 23 Juni, 2024.

Akitoa salamu za rambirambi, Mheshimiwa Waziri Tax ameelezea kuguswa na msiba huo na kusema kuwa Taifa limepoteza Shujaa aliyelitumikia Taifa kwa Umahiri Mkubwa, na Marehemu Brigedia Jenerali Chakila ameacha pengo kubwa kwa familia yake na Taifa kwa ujumla, na akatoa kutoa pole kwa Mke wa marehemu Brigedia Jenerali Chakila, familia, ndugu na marafiki.

Aidha akatoa pole kwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Jacob Mkunda, kwa niaba ya Wanajeshi wote wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
 

Attachments

  • IMG-20240626-WA0066.jpg
    IMG-20240626-WA0066.jpg
    589.7 KB · Views: 12
  • IMG-20240626-WA0063.jpg
    IMG-20240626-WA0063.jpg
    526 KB · Views: 13
  • IMG-20240626-WA0060.jpg
    IMG-20240626-WA0060.jpg
    536.1 KB · Views: 15
  • IMG-20240626-WA0054.jpg
    IMG-20240626-WA0054.jpg
    414.9 KB · Views: 15
  • IMG-20240626-WA0051.jpg
    IMG-20240626-WA0051.jpg
    333.4 KB · Views: 16
  • IMG-20240626-WA0050.jpg
    IMG-20240626-WA0050.jpg
    364.3 KB · Views: 17
  • IMG-20240626-WA0042.jpg
    IMG-20240626-WA0042.jpg
    453.8 KB · Views: 18
  • IMG-20240626-WA0070.jpg
    IMG-20240626-WA0070.jpg
    280.1 KB · Views: 15
Aiseee nimemuona Mama mzuri Waziri wa Ulinzi poleni jeshi
 
Back
Top Bottom