Waziri wa Ulinzi wa Afrika Kusini akatwa mshahara kwa matumizi ya ndege ya Jeshi

Waziri wa Ulinzi wa Afrika Kusini akatwa mshahara kwa matumizi ya ndege ya Jeshi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rais wa Afrika Kusini amemkata mshahara waziri wa ulinzi kwa miezi mitatu baada ya kuruhusu maafisa wa chama tawala kusafari kwa kutumia ndege ya jeshi hadi nchini Zimbambwe pamoja naye Septemba 9.

1601279905482.png
Nosiviwe Mapisa-Nqakula alishtumiwa kwa kuruhusu matumizi ya rasilimali ya taifa kwa sababu za siasa za chama.

Jeshi la nchi hiyo lilikuwa limeeleza kwamba waziri huyo alikuwa katika ziara rasmi ya kitaifa na kwamba aliwafanyia abiria wengine hisani kwa kuwabeba.
Lakini Rais Cyril Ramaphosa aliitaja hatua hiyo kama makosa.

Bi. Mapisa-Nqakula alienda mji mkuu wa Zimbambwe, Harare kuhudhuria mkutano uliokuwa umepangiwa kujadili masuala ya kanda.

Ujumbe kutoka chama tawala cha Afrika Kusini - African National Congress (ANC) - ulikuwa unahudhuria mkutano huo kwa mazungumzo ya dharura na chama tawala cha Zimbambwe Zanu-PF lengo lao likiwa ni kutatua mgogoro wa kisiasa na kiuchumi nchini humo.

Lakini wasasiasa wa upinzani walimkosoa vikali waziri huyo kwa sababu aliandamana na ujumbe wa chama cha ANC.

Bwana Ramaphosa, ambaye kipindi anaingia madarakani aliahidi kumaliza sifa mbaya ya chama cha ANC baada ya mwongo mmoja wa kashfa za ufisadi, alisema kwamba "kwa kuandamana na wajumbe wa ANC kwa ndege aliokuwa anatumia, hakufanya uamuzi stahiki unaozingatia uongozi mzuri".

Matokeo yake, alisema ameamua kumkata mshahara Bi. Mapisa-Nqakula na pesa hizo zitaelekezwa katika mfuko wa kusaidia kukabiliana na janga la corona.

Wakati huo huo, chama cha upinzani cha Democratic Alliance kilisema hatua iliyochukuliwa na Bwana Ramaphosa haitoshi.

Suala hilo huenda likajadiliwa zaidi bungeni huku kukiwa na wito wa waziri huyo kufutwa kazi.
 
Bi. Nosiviwe Mapisa-Nqakula waziri wa ulinzi Afrika Kusini amekatwa mshahara wake wa miezi mitatu baada ya kuruhusu maafisa wa chama tawala kusafiri naye kwa kutumia ndege ya jeshi hadi nchini Zimbambwe.

Bi Mapisa alikuwa ameenda katika ziara rasmi ya kitaifa huku akiwafanyia abiria wengine hisani kwa kuwabeba.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alisema waziri huyo alitumia rasilimali ya taifa kwa sababu za siasa za chama.

Suala hilo huenda likajadiliwa zaidi bungeni huku kukiwa na wito wa waziri huyo kufutwa kazi.

BBC Swahili

Kuna Chama kimoja hivi Afrika Mashariki 'nimekisahau' chenyewe 'Mali' au 'Rasilimali' za Taifa 'imeshazirasimisha' kuwa ni zake tokea 'Kishike' Dola.
 
Huyo rais wa Afrika Kusini si mchezo! Ametoa fundisho kwa mawaziri wengine
 
Huyo rais wa Afrika Kusini si mchezo! Ametoa fundisho kwa mawaziri wengine
Huyo Ramaphosa hakuna kitu hapo,sio mkali wala nini ni vile tu ameona kelele zimekua nyingi akaona nae azuge tu.
 
Wee acha
Bi. Nosiviwe Mapisa-Nqakula waziri wa ulinzi Afrika Kusini amekatwa mshahara wake wa miezi mitatu baada ya kuruhusu maafisa wa chama tawala kusafiri naye kwa kutumia ndege ya jeshi hadi nchini Zimbambwe.

Bi Mapisa alikuwa ameenda katika ziara rasmi ya kitaifa huku akiwafanyia abiria wengine hisani kwa kuwabeba.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alisema waziri huyo alitumia rasilimali ya taifa kwa sababu za siasa za chama.

Suala hilo huenda likajadiliwa zaidi bungeni huku kukiwa na wito wa waziri huyo kufutwa kazi.

BBC Swahili

Kuna Chama kimoja hivi Afrika Mashariki 'nimekisahau' chenyewe 'Mali' au 'Rasilimali' za Taifa 'imeshazirasimisha' kuwa ni zake tokea 'Kishike' Dola.
weee acha tu 😂
 
Huyo Ramaphosa hakuna kitu hapo,sio mkali wala nini ni vile tu ameona kelele zimekua nyingi akaona nae azuge tu.
Ramaphosa anajionea mapichapicha, yeye analinda interest zake za kibiashara zisije guswa.

Maybe wanahitaji raisi mzungu tena kuwachangamsha, kuna kitu ndani ya kinasaba cha sisi weusi kinachotufanya tuwe wabinafsi sana.

Kuna mmoja alisema kwani akifa kiwanja atazikwa nacho..

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Kweli Kapuya naye aliwahi kutumia ndege ya Jeshi kwa mambo tofauti ila bahati yake wakati ule mitandao haikuwa kama leo
 
Back
Top Bottom