Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Unaweza kudhani kuwa nchi kubwa kama China, masuala ya rushwa yangekuwa yameshaisha lakini mambo bado yanatokota.
Hivi karibuni baadhi ya maafisa wa Marekani wameliambia gazeti la Financial Times kwamba Waziri wa Ulinzi wa China Dong Jun yupo kwenye Uchunguzi mzito kufuatia madai ya rushwa yanayomkabili.
Kama ripoti hii ya Financial Times itakuwa ni kweli basi Dong Jun atakuwa ni Waziri wa tatu wa China kuchunguzwa kutokana na madai ya rushwa.
Alipoulizwa kuhusu madai ya uwepo wa madai ya kwamba Waziri Dong Jun yupo kwenye uchunguzi mzito, msemaji wwa Wizara ya Mambo ya Njee Mao Ning amedokeza kuwa ripoti hiyo ya Financial Times ni ya uongo.
Ikumbukwe kuwa tangu mwaka jana takriban wanajeshi 9 kutoka Jeshi la China walihusishwa na madai ya rushwa huku Mabosi wa kampuni ya aerospace wakiwa wametolewa kwenye nafasi zao za uongozi.
Waziri Dong Jun aliteuliwa kuwa Waziri Desemba 2023 baada ya Li Shangfu Waziri aliyekuwa kabla yake kuondolewa kwenye nafasi hiyo baada ya miezi 7.
Kufikia sasa bado haijaelezwa kwa kina ni madai gani hasa ya rushwa Waziri Dong Jun anakabiliwa nayo.
Soma pia: Mwenyekiti wa zamani wa benki ya China ahukumiwa kifo
China kwa sasa imeonekana kuchukua hatua kali kwa viongozi wote wanaokabiliwa na mashtaka ya ufisadi kama ambavyo ilionekana siku chache nyuma baada ya Mwenyekiti wa Bank Of China kupewa adhabu ya kifo baada ya kupatikana na hatia ya kuchukua rushwa ya USD Milioni 16.8 kutoka kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali waliokuwa wanataka kuchukua mikopo kutoka kwenye benki hiyo.
Tuhuma za rushwa na ufisadi zimekuwa zikiwakabili Mawaziri mbalimbali duniani.
Barani Afrika, mwezi Juni mwaka 2024 Waziri wa Michezo wa Africa Kusini Zizi Kodwa alilazimika kujiuzulu baada ya kukabiliwa na tuhuma za kupokea rushwa ya takriban USD 85,000 kutoka kwa mfanyabiashara Jehan Mackay.
Kodwa alipokea fedha hizo ili KUTOKA kwa Mackay ili kumuwezesha Mackay kupata tenda ya kuweka huduma ya software kwenye mji wa Johanesburg.
Hivi kwa Tanzania hii level ya uwajibikaji tunayo kweli? Lini ni mara ya mwisho tumesikia Waziri au kigogo mkubwa serikalini amewajibishwa kwa madai ya rushwa na ufisadi? Au serikali yetu ni safi kiasi hicho?
=============================================================
China's Defence Minister Dong Jun has been placed under investigation as part of a wide-ranging anti-corruption probe, the Financial Times (FT) reported on Wednesday (Nov 27), citing current and former US officials.
If FT's report is confirmed, Dong would be the third consecutive serving or former Chinese defense minister to be investigated for alleged corruption.
At a regular news briefing, Chinese foreign ministry spokesperson Mao Ning said in a response to a question about the FT report that it was "just shadow-chasing".
China's military has undergone a sweeping anti-corruption purge since last year, with nine People's Liberation Army (PLA) generals and at least four aerospace defense industry executives removed from the national legislative body to date.
Dong, a former PLA Navy chief, was appointed defense minister in December 2023. His predecessor, Li Shangfu, was removed after seven months on the job.
As defence minister, Dong is responsible for China's military diplomacy with other nations. He oversaw a recent thaw in US-China military-to-military ties, with both nations holding theatre-level commander talks for the first time in September.
Source: Reuters, Chanel News Asia