Waziri Wa Viwanda Kenya Ajiuzulu

Waziri Wa Viwanda Kenya Ajiuzulu

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
3,068
Reaction score
277
Waziri wa Ustawishaji wa Viwanda nchini Kenya, Henry Kosgey, ambaye alikuwa amepangiwa kufikishwa maakamani na maafisa wa taasisi ya kupambana na rushwa, amejiuzulu wadhifa wake.

Kosgey amechukuwa hatua hiyo siku moja baada ya Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Kenya, Amos Wako kutoa idhini kwa tume ya kupambana na ufisadi nchini humo, kumkamata na kumfungulia mashtaka kutokana na kashfa ya kuruhusu uagizaji wa magari yaliyopita muda wa kutumika nchini humo.

Bwana Kosgey ni mwenyekiti wa chama cha ODM cha Waziri Mkuu Raila Odinga na pia ni mmoja wa Wakenya sita wanaoshutumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu, ICC, kupanga machafuko baada ya uchaguzi miaka mitatu iliyopita.

Chama cha ODM hata hivyo kimesema kitaendelea kumuunga mkono Kosgey.(BBC Swahili)
 
Back
Top Bottom