Wazo ftatu: Serikali iandae sera ya kuhamasisha ndoa (iwalipie mahari waoaji kwa asilimia kadhaa) ili kukuza uchumi wa Taifa

Wazo ftatu: Serikali iandae sera ya kuhamasisha ndoa (iwalipie mahari waoaji kwa asilimia kadhaa) ili kukuza uchumi wa Taifa

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Wakuu mpo?

Kwa wale mlio na familia namaanisha mke na watoto nadhani mtanielewa kwa haraka,

Mtu aliyeoa mwenye majukumu, mwenye afya njema ni nadra sana kumkuta kalala ndani bila kujishughulisha na kazi yeyote, wengi huamka asubuhi huenda kazini na kurudi home mida mibovu, sababu kubwa ni majukumu (kulea familia, kulipa kodi, bili na gharama za matibabu),

Hii ni tofauti kabisa kwa wasio na familia wengi hukaa bila kujishughulisha na chochote,

Taifa linaundwa na watu, familia moja + familia nyingine + familia + = Taifa

Sasa ili kila raia mwenye afya njema awajibike bila kusukumwa na yeyote ashiriki katika shughuli za uzalishaji inabidi awe na majukumu, na majukumu menyewe ni kuwa na familia.

Uzalishaji wa mali na huduma utaongezeka (domestic production)

Matumizi ya ndani yataongezeka (domestic expenditure) mzunguko pia wa pesa utakuwepo
, Uchumi utakuwa kwa kasi.

Je kila Mtanzania mtu mzima akihamasishwa aoe tutaondoa kundi la watu wasiojishughulisha na kuongeza ukuaji wa uchumi?
 
Kwani unafikiri shida ni mahari? na chakula ndani ya familia serikali itawanunulia? vijana hawana ajira maisha yataendaje, hawana chochote cha kuwaingizia vipato mtaani watawatunzaje watoto wa watu?
 
Kwani unafikiri shida ni mahari? na chakula ndani ya familia serikali itawanunulia? vijana hawana ajira maisha yataendaje, hawana chochote cha kuwaingizia vipato mtaani watawatunzaje watoto wa watu?
Hujaelewa huu uzi mkuu
 
Kwani ndege ya kwenda marekani nauli ni shingapi? au hata ya kwenda kongo. Ni vema tukajichanga mapema.
 
Kwahiyo mkuu unaamini kataa ndoa wanaogopa mahali? No way.
 
Back
Top Bottom