Wazo Fyatu: Ni mabingwa wa kuzindua vitu

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Haiwezekani hata mwezi haujapita watu washaanza kulalamikia SGR, yaani uhamasishaji wote wa kwanini hii ni reli ya kisasa. Kumbe bado ina watu wa kizamani!! Wanafikra za kizamani.

Imenikumbisha Wabongo tunavyopenda kuzindua vitu. Angalia vitu vilivyozinduliwa kwa mbwembwe za mbio za mwenge. Angalia uwanja wa Julius Nyerere International Airport ulivyozinduliwa lakini si muda watu wakalalamikia maji sijui vyoo.

Kama huamini angalia mabasi ya mwendo kasi. Angalia maofisi na mahospitali, yaani tumezoea vitu vichafu kiasi kwamba vitu vizuri tunaona vya "kizungu"! Labda tuache kuzindua kwa mbwembwe.

Shida kwelikweli!
 
Bongo hakuna watu mkuu. Bali Kuna mifano ya watu. Watoto wanafundishwa usafi tangu wakiwa chekechea Hadi vyuo vikuu (takribani miaka 20). Cha kushangaza wakiwa watu wazima bado hawajui usafi.Sasa utasema kuwa hawa ni watu kweli? Shame on us!
 
Unaambiwa uwanja wa mkapa ulifanyiwa ukarabati mkubwa mpaka wi-fi ya bure ikawekwa saivi sijui imepotelea wapi

Uwanja wa mpira wa Dodoma sijui nao umefikia wapi? Nilimuonaga majaliwa ITV anabeba zege mwaka 2019 kama sikosei
 
"akili zilezile za zamani", hili ni neno kubwa sana.

Tunakimbilia kwenye technolojia na Dunia ya sasa huku tukitegemea watu wale wale wenye akili za zamani zilizochakaa.
 
Unaambiwa uwanja wa mkapa ulifanyiwa ukarabati mkubwa mpaka wi-fi ya bure ikawekwa saivi sijui imepotelea wapi

Uwanja wa mpira wa Dodoma sijui nao umefikia wapi? Nilimuonaga majaliwa ITV anabeba zege mwaka 2019 kama sikosei
Halafu watu washazoea tayari...
 
Bongo hakuna watu mkuu. Bali Kuna mifano ya watu. Watoto wanafundishwa usafi tangu wakiwa chekechea Hadi vyuo vikuu (takribani miaka 20). Cha kushangaza wakiwa watu wazima bado hawajui usafi.Sasa utasema kuwa hawa ni watu kweli? Shame on us!
Ila wakitia viwalo vyao utadhani ni watu kwelikweli...
 
ukitaka jambo lako life vibaya peleka mwenge ukazindue mkuu nakupa mwaka mmoja tu kama ni kiwanda kinakufa Kama ni sehemu ya huduma zinakata chap yaani ukijichanganya na mwenge unamulika mpka watu wanakimbia
 
Mojawapo tunavyovizindua vizuri ni barabara na visima vya maji...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…