Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,641
- 11,958
Kwanza naomba nitangulize kuomba radhi wale wote ambao nitawakwaza kwa wazo langu hili, Ila naomba tu ileleweke kuwa nimetumia tu haki yangu ya kikatiba kutoa maoni.
Kwa kifupi sana ni kwamba kilichopo nyuma ya hii changia changia inayo endeshwa na CHADEMA kutunisha mfuko wa kampeni ina kitu kikubwa nyuma yake na si Kama hivyo ambavyo wengi wanaymvyoichukulia.
CHADEMA wanafanya hivyo makusudi kwa lengo la kuzima hisia mbaya zinazoanza kujengeka na kuaminika miongoni mwa watanzania ambao ndio wapiga kura kwamba CHADEMA na mgombea wao wanafadhiliwa na kupewa mahela mengi na mataifa makubwa ya nje (mabepari) kwa lengo la kupambana na serikalini ya Magufuli ambayo si rafiki kwa watu hao.
Sasa ili kuzima kabisa hisia hizo CHADEMA wanafanya uchangishaji huu ili kuaminisha watu kuwa hawana pesa hivyo kauli ya kwamba wanalipwa itakosa mashiko.
Haki ni mbinu nzuri sana hii na hadi sasa nadhani imefanikiwa kwa asilimia kubwa na wengi tayari wamenasa mtegoni.
Haiingii akilini kabisa eti mhe Tundu Lissu mtu makini kabisa akubali kurudi Tanzania kuja ku risk maisha yake huku akiwa hana pesa za kampeni?!! Hapana kabisa hili haliwezekani asingerudi huku kwasababu naamini hakuna asicho kijua kuhusu chama chake jinsi financial power yake ilivyo, hawezi kuja kugombea Urais kwa kutegemea michango ya walalahoi hata mara moja.
Lengo kuu la changia changia ni kuzima tuhuma za kulipwa na mabepari ili kuivuruga Tanzania na ikiwezekana kushika dola (puppet).
Ni wazo langu tu wandugu nawe waweza toa lako.