Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Nishati ni muhimu sana katika Nchi na Tanzania kama nchi ya kitropiki imebarikiwa kuwe na Jua la kutosha ukiunganisha na vyanzo vingine vingi, vilevile kutokana na Vyanzo vya Maporomoko Nishati ya Jua inaweza ikaunganishwa na Maporomoko ya Maji ili kutengeneza battery ya kutunzia Nishati inayozalishwa (Pumped Hydro); Jinsi ya mfumo unavyofanya kazi nimeshauzungumzia kwenye Nyuzi nyingine.
Ila kwa ufupi ni kila nyumba kuwa connected na panels ambazo zitazalisha umeme na kuingizwa kwenye Grid; malipo kwa mzalishaji itakuwa ni kitu kinaitwa Net Metering ukizalisha zaidi Tanesco wanachukua ziada (inakupa credit) siku ukitumia umeme mwingi kuliko uzalishaji basi unakatwa kulingana na credit zako. Mfumo huu kwa mzalishaji utakuwa wa gharama ndogo sana sababu sasa hivi panels zimeshuka sana bei na nchi nyingi zinatoa ruzuku kwenye green energy; pia mfumo huu mtu hatakuwa na uhitaji wa battery.
Assumption:
Nyumba ina Panels Nne; Na Makadirio ya Kutoa 8kwh (Units Nane kwa Siku)
Kutokana na Sensa ya 2023
Tanzania ina makazi 14,152,803
Kwahio kama Nyumba hizo zitakuwa na panels nne kwa makadirio ya kuzalisha units Nane kwa siku; hivyo kuna uwezekano / capacity ya Watanzania / Wamiliki wa Nyumba kuwa wazalishaji wa Umeme na kuzalisha 113,222,424KW sawa na 113,222MW sawa na 113.2GW
Tunaongea kila siku watanzania binafsi kuingia UBIA na Serikali katika maendeleo na nadhani hakuna maendeleo kama ya kuhakikisha Nishati inapatikana na bila kutumia maeneo mahekari na mahekari ya kuweka solar panels.
Pia Tanesco itaendelea kuwa msambazaji wa kusambaza nishati inayozalisha na kukusanya kutoka kwa wazalishaji mbalimbali (so long as bei yao ni ndogo kuliko wanavyoweza kuzalisha wenyewe)

Tuanzie Tulipo, Tutumie Tulichonacho, Tufanye Tunachoweza